22-Kitaab At-Tawhiyd: Nabiy Alivyohami Tawhiyd Kufunga Kila Njia Ipelekayo Kwenye Shirki

Mlango Wa 22

بَابُ مَا جَاءَ فِي حِمَايَةِ النَّبِي صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ جَنَابَ اَلتَّوْحِيدِ وَسَّدِّهِ كُلَّ طَرِيقٍ يُوَصِّلُ إِلَى اَلشِّرْكِ

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alivyohami Tawhiyd Na Kufunga Kwake

Kila Njia Ipelekayo Kwenye Shirki


 

 

وَقَوْلِ اَللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

 لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢٨﴾

((Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini (muongoke) mwenye huruma kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rahmah))

 

 فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ﴿١٢٩﴾

((Na wakikengeuka, basi sema: “Amenitosheleza Allaah; Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye. Kwake nimetawakali. Naye ni Rabb wa ‘Arsh adhimu)) [At-Tawbah (9: 128-129)]

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لاَ تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ قُبُورًا، وَلاَ تَجْعَلُوا قَبْرِي عِيدًا، وَصَلُّوا عَلَيَّ فَإِنَّ صَلاتَكُمْ تَبْلُغُنِي حَيْثُ كُنْتُمْ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ وَرُوَاتُهُ ثِقَاتٌ

Imepokelewa toka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Msifanye nyumba zenu makaburi, wala msilifanye kaburi langu kuwa ni pahala pa kurejewa rejewa na niswalieni, kwani kuniswalia kwenu kunanifikia popote mlipo)) [Abuu Daawuwd kwa isnaad Hasan ya wasimuliaji wanaotegemewa]

 

وَعَنْ عَلِيِّ بْنِ الْحُسَيْنِ: أَنَّهُ رَأَى رَجُلاً يَجِيءُ إِلَى فُرْجَةً كَانَتْ عِنْدَ قَبْرِ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَيَدْخُلُ فِيهَا فَيَدْعُو، فَنَهَاهُ وَقَالَ أَلاَ أُحَدِّثُكُمْ حَدِيثًا سَمِعْتُهُ مِنْ أَبِي عَنْ جَدِّي عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لاَ تَتَّخِذُوا قَبْرِي عِيدًا وَلاَ بُيُوتَكُمْ قُبُورًا،  وَصَلُّوا عَلَيَّ فَإِنَّ تَسْلِيمَكُمْ لَيَبْلُغُنِي أَيْنَ كُنْتُمْ)) رَوَاهُ فِي   الْمُخْتَارَةَ

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aliy bin Al-Husayn kwamba alimwona mtu akitoka kwenye upenyo uliokuwa katika ukuta wa kaburi la Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiingia na kuomba. Akamzuia akamwambia: Nikujulishe Hadiyth nilioisikia kutoka kwa baba yangu kutoka kwa babu yangu kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Msifanye kaburi langu kuwa ni pahala pa kurejewa rejewa, wala [msifanye] nyumba zenu makaburi, [kwa kutokuswali ndani yake] na niswalieni kwenu kuniswalia kunanifikia popote mlipo)) [Al-Mukhtaar – mkusanyo wa Hadiyth za Imaam Al-Maqdisiyy Al-Hanbaliyyi]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Baraa-ah (At-Tawbah 9:128-129)).

 

2-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alifanya juhudi kubwa kuweka Ummah huu mbali na khatari ya shirki kadiri iwezekanavyo.         

 

3-Kujali kwake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mafaniko yetu, furaha, amani na huruma yake kwetu.

 

4-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amekataza kuzuru kaburi lake kwa namna fulani (isiyopasa ki shariy’ah) ingawa kuzuru kaburi lake ni miongoni mwa ‘amali njema kabisa.

 

5-Makatazo ya kukithirisha mno kuzuru kaburi lake.

 

6-Himizo lake la kuswali Nawaafil (Swalaah za Sunnah) nyumbani.

 

7-Maswahaba wamekiri na kukubaliana kwamba kuswali makaburini imekatazwa.

 

8-Maelezo kwamba kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kunamfikia hata kama mtu yuko mbali vipi. Kwa hiyo hakuna haja ya kulikuribia sana kaburi lake kumtakia rahmah na amani kama inavyodhaniwa kimakosa.

 

9-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) yuko katika maisha ya Al-Barzakh ambako huonyeshwa ‘amali za ummah wake pamoja na swalaatu was-salaamu ‘alayhi (kumtakia rahmah na amani).

 

 

 

Share