23-Kitaab At-Tawhiyd: Baadhi Ya Ummah Huu Wataabudu Masanamu

 

Mlango Wa 23

بَابُ مَا جَاءَ أَنَّ بَعْضَ هَذِهِ الْأُمَّةِ يَعْبُدُ الْأَوْثَانَ

Baadhi Ya Ummah Huu Wataabudu Masanamu

 


 

 

 

وَقَوْلُهُ تَعَالَى:

Na kauli Yake Ta’aalaa:

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ  

((Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti)) [An-Nisaa (5: 51)]

 

وَقَوْلُهُ تَعَالَى :

Na kauli Yake Ta’aalaa:

 

قُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ مَن لَّعَنَهُ اللَّـهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ الْقِرَدَةَ وَالْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ الطَّاغُوتَ ۚ  

((Sema: “Je, nikujulisheni la shari zaidi kuliko hayo kwa malipo (mabaya) mbele ya Allaah?” Yule ambaye Allaah Amemlaani na Akamghadhibikia na Akawafanya miongoni mwao manyani na nguruwe na wakaabudu twaghuti)) [Al-Maaidah (5: 60)]

 

وَقَوْلُهُ تَعَالَى:

Na kauli Yake Ta’aalaa:

قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَىٰ أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِم مَّسْجِدًا ﴿٢١﴾

((Wakasema wale walioshinda katika shauri lao: “Bila shaka tutajenga Msikiti juu yao)) [Al-Kahf (18: 21)]

 

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لَتَتَّبِعُنَّ سُنَنَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ حَذْوَ الْقُذَّةِ  بِالْقُذَّةِ، حَتَّى لَوْ دَخَلُوا جُحْرَ ضَبٍّ لَدَخَلْتُمُوهُ)) قَالُوا: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! الْيَهُودُ وَالنَّصَارَى؟ ؟قَالَ: ((فَمَنْ؟)) - أَخْرِجَاهُ

Imepokelewa kutoka kwa kwa Abuu Sa'iyd (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Bila shaka mtafuata nyendo za watu waliokuwa kabla yenu, hatua kwa hatua hata wakiingia kwenye shimo la kenge nanyi mtaingia)). Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah, je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara?" Akasema: ((Nani basi [kama si hao]?)) [Al-Bukhaariy na Muslim]  

 

وَلِمُسْلِمٍ عَنْ ثَوْبَانَ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ: ((إِنَّ اَللَّهَ زَوَى لِيَ الأَرْضَ، فَرَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا،  وَإِنَّ أُمَّتِي سَيَبْلُغُ مُلْكُهَا مَا زُوِيَ لِي مِنْهَا. وَأُعْطِيتُ الْكَنْزَيْنِ الأَحْمَرَ وَالأَبْيَضَ. وَإِنِّي سَأَلْتُ رَبِّي لأُمَّتِي أَنْ لاَ يُهْلِكَهَا بِسَنَةٍ بِعَامَّةٍ، وَأَنْ لا يُسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُّوا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ، فَيَسْتَبِيحَ بَيْضَتَهُمْ، وَإِنَّ رَبِّي قَالَ: يَا مُحَمَّدُ إِنِّي إِذَا قَضَيْتُ قَضَاءً فَإِنَّهُ لاَ يُرَدُّ، وَإِنِّي أَعْطَيْتُكَ لأُمَّتِكَ أَنْ لا أُهْلِكَهُمْ بِسَنَةٍ ِعَامَّةٍ، وَأَنْ لا أُسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُّوا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ فَيَسْتَبِيحَ بَيْضَتَهُمْ، وَلَوْ اِجْتَمَعَ عَلَيْهِمْ مَنْ بِأَقْطَارِهَا حَتَّى يَكُونَ بَعْضُهُمْ يُهْلِكُ بَعْضًا، وَيَسْبِيَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا))

Na Muslim amerekodi kutoka kwa Thawbaan (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika Allaah Amenikusanyia ardhi [dunia] nikaona Mashariki yake na Magharibi yake. Na hakika Ummah wangu utaenea na kumiliki vyote vilivyo katika sehemu hizo nilokusanyiwa. Na nimepewa hazina mbili; nyekundu [Ufalme wa Kirumi] na nyeupe [Ufalme wa Kifursi]. Hapo nikamuomba Rabb wangu Asijaalie Ummah wangu kuangamizwa kwa baa kuu la jumla na usitekwe na adui ajnabi atakayeuharibu mjii mkuu wao na kuuangusha uongozi wao.  Rabb wangu Akajibu:  Ee Muhammad! Nikihukumu amri basi hakika hairudi. Nimekadiria kwamba Ummah wako hautahiliki mara moja kwa baa kuu la jumla na kwamba hautatekwa na adui ajnabi na kuharibu mjii mkuu wao na kuuangusha uongozi wao, ila kundi moja la Ummah wako litahilikisha makundi mengine au kuwafanya mateka)) [Muslim]

 

وَرَوَاهُ الْبَرْقَانِيُّ فِي صَحِيحِهِ وَزَادَ: ((وَإِنَّمَا أَخَافُ عَلَى أُمَّتِي الأَئِمَّةَ الْمُضِلِّينَ، وَإِذَا وَقَعَ عَلَيْهِمْ اَلسَّيْفُ لَمْ يُرْفَعْ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَلا تَقُومُ اَلسَّاعَةُ حَتَّى يَلْحَقَ حَيٌّ مِنْ أُمَّتِي بِالْمُشْرِكِينَ وَحَتَّى تَعْبُدَ فِئَامٌ مِنْ أُمَّتِي الأَوْثَانَ، وَإِنَّهُ سَيَكُونُ فِي أُمَّتِي كَذَّابُونَ ثَلاثُونَ كُلُّهُمْ يَزْعُمُ أَنَّهُ نَبِيٌّ، وَأَنَا خَاتَمُ اَلنَّبِيِّينَ لا نَبِيَّ بَعْدِي وَلا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي عَلَى الْحَقِّ مَنْصُورَةٌ لا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ وَلا مَنْ خَالَفَهُمْ حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اَللَّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى))

Na Al-Barqaaniyy katika Swahiyh yake akaongezea yafuatayo: ((Bali nnachokikhofia kwa Ummah wangu ni kupotezwa na viongozi wapotofu ambao wakiangukiwa na upanga, upanga huo hautonyanyuliwa hadi Siku ya Qiyaamah. Wala Qiyaamah hakitafika mpaka baadhi ya Ummah wangu wawafuate makafiri na waanze kuabudu masanamu. Nawakhofia watakuja miongoni mwao manabii wa uongo thelathini; kila mmoja anadai kuwa yeye ni nabiy na hali mimi ni Nabiy wa mwisho hakuna baada yangu. Lakini kundi moja katika ummah wangu litabakia kuwa katika haki na ushindi, hlitodhurika kwa kuanguka kwa wengine mpaka ifike amri ya Allaah Tabaraka wa Ta’aalaa)) [Al-Barqaaniy fiy Swahiyhih]  

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah An-Nisaa (4: 5).

 

2-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Maaidah (5: 60).

 

3-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Kahf (18: 21).

 

4-Jambo muhimu kabisa kuhusu maana ya Al-jibt na Atw-Twaaghuwt katika maudhui hii. Je, ni kuitakidi kwa moyo, au kukubaliana tu na wale wanaofanya (shirki) na hali wanachukia na kujua kwamba ni upotofu?

 

5-Mayahudi kudai kwamba (Makafiri Quraysh) wanaotambua hakika ya kufru yao kwamba wako katika uongofu zaidi kuliko Waumini.

 

6-   Watu kama hao (watakaopotea na kuabudu masanamu) wanapatikana katika Ummah huu wa Kiislamu kama ilivyotajwa katika Hadiyth ya Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه). Hii ndio maudhui kuu ya mlango huu.

 

7-Utabiri wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba wengi katika Ummah wake wataabudu waabudiwa wa uongo (masanamu n.k.).

 

8-La ajabu zaidi ni kutokeza kwa wale wanaodai unabiy kama Al-Mukhtaar[1] juu ya kuwa alikiri shahaadah na kukiri kwake kwamba ni miongoni mwa Ummah wa Kiislamu, na (kukiri kwake) kwamba Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ni haki na Qur-aan ni haki, na kukiri kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Nabiy wa mwisho. Lakini inashangaza kwamba muongo kama huyo anajidai unabiy na huku anaaminiwa juu ya kudhihirika kwake kupinga shahaadah yake. Al-Mukhtaar alitokeza katika kipindi cha mwisho wa Maswahaba na akapata wafuasi wengi.

 

9-Bishara njema kwamba haki haitopotea moja kwa moja kama zamani, bali litabaki kundi moja litakalobakia katika haki.

 

10-Alama kubwa kabisa ni kwamba wao (kundi la haki) hawatodhuriwa na waliowakhalifu wala wapinzani japokuwa wao watakuwa wachache.

 

11-Hali hiyo ndivyo itakavyokuwa hadi Qiyaamah.

 

12-Bishara ya miujiza kadhaa kutokana na kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) miongoni mwazo ni:

  • Kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Alimdhihirishia ardhi Mashariki na Magharibi na kumbainishia maana ya bishara hiyo na hakika imetokea kama alivyojulisha, si Kaskazini wala Kusini.
  • Kwamba Ametunukiwa hazina mbili (Rome na Persia). 
  • Kwamba du’aa zake mbili kwa ajili ya Ummah zimetakabaliwa.
  • Kwamba du’aa yake ya tatu haikukubaliwa.
  • Kwamba utakapoanguka upanga (vita), basi vita hivyo havitosimama, akahadithia kuhusu baadhi ya Ummah huu kuangamiza baadhi yake.
  • Utabiri wake wa manabii ya uongo katika Ummah wake.
  • Kwamba daima kutakuweko kundi la ushindi.
  • Kwamba yote hayo yalitokea kama alivyojulisha japokuwa kila moja ya hayo yalionekana mbali kuyakinika akilini.

 

13-Khofu yake kubwa kwa Ummah wake kutokana na viongozi wapotofu.

 

14-Kutahadharisha na tanbihi ya maana ya ‘ibaadah ya masanamu.

           

 

[1] Al-Mukhtaar bin Abiy ‘Ubayd Ath-Thaqafiy aliyeitawala Kuwfaa mwanzo wa Khilaafah ya Ibn Zubayr.

 

 

Share