36-Kitaab At-Tawhiyd: Riyaa – Kujionyesha

Mlango Wa 36

بَابٌ مَا جَاءَ فِي الرِّيَاءِ

Riyaa – Kujionyesha


 

وَقَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ﴿١١٠﴾

((Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni mtu kama nyinyi, nafunuliwa Wahy kwamba: Hakika Muabudiwa wa haki wenu ni Ilaah Mmoja Pekee. Hivyo anayetaraji kukutana na Rabb wake, basi na atende ‘amali njema na wala asishirikishe yeyote katika ‘ibaadah za Rabb wake”)) [Al-Kahf: (18:110)]

 

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ مَرْفُوعًا: ((قَالَ تَعَالَى: أَنَا أَغْنَى الشُّرَكَاءِ عَنِ الشِّرْكِ مَنْ عَمِلَ عَمَلاً أَشْرَكَ مَعِي فِيهِ غَيْرِي تَرَكْتُهُ وَشِرْكَهُ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Na kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) Hadiyth Marfuw’: ((Allaah Ta’aalaa Amesema: Mimi ni mwenye kujitosheleza, sihitaji washirika. Kwa hiyo, yule afanyae ‘amali hali ya kumshirikisha mwengine ndani yake pamoja na Mimi nitamuachilia mbali na shirki yake)) [Muslim]

 

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ مَرْفُوعًا: ((أَلا أُخْبِرُكُمْ مَا هُوَ أَخْوَفُ عَلَيْكُمْ عِنْدِي مِنَ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ؟)) قَالُوا بَلَى: قَالَ: ((الشِّرْكُ الْخَفِيُّ، يَقُومُ الرَّجُلُ فَيُصَلِّي فَيُزَيِّنُ صَلاتَهَ، لِمَا يَرَى مِنْ نَظَرِ رَجُلٍ إِلَيْه)) رَوَاهُ أَحْمَدُ

Na Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd, Hadiyth Marfuw’: ((Je, niwajulisheni nikikhofiacho zaidi juu yenu kuliko hata Masiyh Ad-Dajjaal?)) Wakasema: Ndio. Akasema: ((Ni shirki iliyojfichikana kama vile mtu kuipamba Swalaah yake kwa kuwa anaangaliwa)) [Ahmad, Ibn Maajah]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Kahf (18: 110).

 

2- Suala kuu kuwa ‘amali njema ikiwa ameshirikishwa Allaah (سبحانه وتعالى) na mwenginewe, ni yenye kukataliwa.

 

3-Sababu ya kukatakaliwa ‘amali kama hiyo ni kujitosheleza Kwake Allaah (سبحانه وتعالى) kikamilifu bila ya kumtemgemea yeyote.

 

4-Sababu nyingine ni kuwa Yeye (Allaah سبحانه وتعالى) ni Mbora wa wote kwa hivo hastahiki kushirikishwa na mwengine katika ‘ibaadah Zake. 

 

5-Khofu aliyokuwa nayo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya Riyaa kwa Maswahaba Wake (رضي الله عنهم).

 

6-Aliieleza Riyaa kwa kupigia mfano anayeswali kwa ajili ya Allaah (سبحانه وتعالى), lakini anaipamba vyema Swalaah yake anapojua kuwa wengine wanamwangalia yeye (kinyume na anapokuwa peke yake).

 

 

 

Share