38-Kitaab At-Tawhiyd: Anayewatii Wanachuoni Na Watawala Katika Kuharamisha Aliyohalalisha Au ...

Mlango Wa 38

بَابٌ مَنْ أَطَاعَ الْعُلَمَاءَ وَالْأُمَرَاءَ فِي تَحْرِيمِ مَا أَحَلَّ اَللَّهُ أَوْ تَحْلِيلِ مَا حَرَّمَهُ فَقَدْ اِتَّخَذَهُمْ أَرْبَابًا

Anayewatii Wanachuoni Na Watawala Katika Kuharamisha Aliyohalalisha Au Kuhalalisha Aliyoharamisha Allaah Kawafanya Ni Waabudiwa


 

وَقَالَ اِبْنُ عَبَّاسٍ: يُوشِكُ أَنْ تَنْزِلَ عَلَيْكُمْ حِجَارَةٌ مِنَ اَلسَّمَاءِ. أَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ) وَتَقُولُونَ قَالَ أَبُو بَكْرٍ وَعُمَرُ؟

Na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Kumekurubia kukuteremkieni mawe (ya adhabu) kutoka mbinguni! Mimi nasema: Amesema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nanyi mnasema: Kasema Abuu Bakr na ‘Umar?!”

 

وَقَالَ الإِمَامُ أَحْمَدُ بْنُ حَنْبَلٍ: عَجِبْتُ لِقَوْمٍ عَرَفُوا الإِسْنَادَ وَصِحَّتَهُ،  وَيَذْهَبُونَ إِلَى رَأْيِ سُفْيَانَ وَاَللَّهُ تَعَالَى يَقُولُ: ((فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ))  أَتَدْرِي مَا الْفِتْنَةُ؟ الْفِتْنَةُ اَلشِّرْكُ لَعَلَّهُ إِذَا رَدَّ بَعْضَ قَوْلِهِ أَنْ يَقَعَ فِي قَلْبِهِ شَيْءٌ مِنَ اَلزَّيْغِ فَيَهْلَكَ.  

Na Imaam Ahmad amesema: “Nastajaabishwa na watu waliojua isnaad [ya Hadiyth] na usahihi wake, lakini wanashikilia rai ya Sufyaan [Ath-Thawry] na hali Allaah Anasema: ((Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo)) [An-Nuwr (24:63)]. Je, unajua hapa ni nini fitnah? Fitnah hapa ni shirki. Huenda kwa kukataa baadhi ya mafundisho yake (صلى الله عليه وآله وسلم), jambo hilo laweza kumletea mtu shaka na upotofu moyoni mwake na ikawa hiyo ni sababu ya kuangamia kwake.”

 

وَعَنْ عَدِيٍّ بْنِ حَاتِمٍ: أَنَّهُ سَمِعَ اَلنَّبِيَّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقْرَأُ هَذِهِ الآيَةَ: ((اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ...)) فَقُلْتُ لَهُ: إِنَّا لَسْنَا نَعْبُدُهُمْ. قَالَ: ((أَلَيْسَ يُحَرِّمُونَ مَا أَحَلَّ اَللَّهُ فَتُحَرِّمُونَهُ وَيُحِلُّونَ مَا حَرَّمَ اَللَّهُ فَتُحِلُّونَهُ؟)) فَقُلْتُ بَلَى. قَالَ: ((فَتِلْكَ عِبَادَتُهُم)) رَوَاهُ أَحْمَدُ وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ

Na Imepokelewa kutoka kwa ‘Adiyy bin Haatim(رضي الله عنه)  kwamba amemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Aayah: ((Wamewafanya Wanachuoni wao mafuqahaa wa dini na Wamonaki wao kuwa ni waabudiwa badala ya Allaah…)) [At-Tawbah (9: 31)] Nikasema: Hakika sisi hatuwaabudu. Akasema: ((Je, kwani hawaharamishi Aliyoyahalalisha Allaah nanyi mkayaharamisha? Na wanahalalisha Aliyoyaharamisha Allaah nanyi mnayahalalisha?)) Nikasema: Ndio. Akasema: ((Basi hivyo ndivyo kuwaabudu)) [Ahmad na At-Tirmidhiy na ameipa daraja ya Hasan]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah An-Nuwr (24: 63).

 

2-Tafsiri ya Aayh katika Suwrah Al-Baraa-ah (At-Tawbah 9: 31).

 

3-Kudhihirisha maana ya ‘ibaadah ambayo ilikanushwa na ‘Adiyy (رضي الله عنه).

 

4-Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ametoa mfano wa Abuu Bakr na ‘Umar; na Imaam Ahmad ametoa mfano wa Sufyaan.

 

5-Hali ilibadilika mno kiasi ambacho kuwaabudu watawa imekuwa ‘amali bora kabisa ijulikanayo kwa jina la Al-Wilaayah. Na kuwaabudu wanachuoni ndio elimu na fiqhi. Kisha, hali ikabadilika tena mpaka kiasi ambacho wakawa wanaabudiwa badala ya Allaah watu ambao si hata katika waja wema na wakaabudiwa ambao ni katika majahili kabisa.   

 

 

Share