39-Kitaab At-Tawhiyd: Kutafuta Hukmu Kinyume Na Allaah Na Rasuli Wake Ni Unafiki

 

Mlango Wa 39

باب: أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ

Kutafuta Hukmu Kinyume Na Allaah Na Rasuli Wake Ni Unafiki

 


 

 

 

قَوْلُهُ تَعَالَى:

Kauli Yake Ta’aalaa:

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿٦٠﴾

((Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako; wanataka wahukumiane kwa twaghuti (ubatilifu) na hali wameamrishwa wakanushe hiyo. Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali))

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا ﴿٦١﴾

((Na wanapoambiwa: “Njooni kwenye yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Rasuli; utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwa mkengeuko))

 

فَكَيْفَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ثُمَّ جَاءُوكَ يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا إِحْسَانًا وَتَوْفِيقًا ﴿٦٢﴾

((Basi itakuwaje utakapowafika msiba kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao? Kisha wakakujia wakiapa “Wa-Allaahi hatukutaka ila mazuri na mapatano”)) [An-Nisaa (4: 60-63)]

 

 وَقَوْلُهُ:

Na kauli Yake:

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ ﴿١١﴾

((Na wanapoambiwa: “Msifanye ufisadi katika ardhi.” Husema: “Hakika sisi ni watengenezaji”)) [Al-Baqarah (2: 11)]

وَقَوْلُهُ:

Na kauli Yake:

وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا

((Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya kutengenea kwake)) [Al-A’raaf (7: 56)]

وَقَوْلُهُ:

Na kauli Yake:

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿٥٠﴾

((Je, wanataka hukumu ya (enzi ya) ujahili? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini)) [Al-Maaidah (5: 50)]

 

 وَعَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعًا لِمَا جِئْتُ بِهِ)) قَالَ النَّوَوِيُّ:حَدِيثٌ صَحِيحٌ رَوَيْنَاهُ فِي كِتَابِ ألْحُجَّة بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ  

Na Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hatoamini mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni kufuata niliyokuja nayo)) [Amesema An-Nawawy: Hadiyth Swahiyh imenukuliwa katika Kitaab Al-Hujjah ikiwa na isnaad Swahiyh]

 

وَقَالَ الشَّعْبِيُّ: كَانَ بَيْنَ رَجُلٍ مِنَ الْمُنَافِقِينَ وَرَجُلٌ مِنَ الْيَهُودِ خُصُومَةٌ. فَقَالَ الْيَهُودِيُّ:  نَتَحَاكَمُ إِلَى مُحَمَّدٍ. عَرِفَ أَنَّهُ لا يَأْخُذُ الرِّشْوَةَ.  وَقَالَ الْمُنَافِقُ: نَتَحَاكَمُ إِلَى الْيَهُود.ِ لِعِلْمِهِ أَنَّهُمْ يَأْخُذُونَ الرِّشْوَةَ. فَاتَّفَقَا أَنْ يَأْتِيَا كَاهِنًا فِي جُهَيْنَةَ فَيَتَحَاكَمَا إِلَيْهِ فَنَزلَ: ((أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ...))

Na Ash-Sha’biyy amesema: Kulitokea ugomvi baina ya Myahudi na Mnafiki. Myahudi akasema: “Tutafute hukmu kwa Muhammad.” Kwani alijua kwamba hapokei rushwa. Na mnafiki akasema: “Tutafute hukmu kwa Mayahudi.” Akijua kwamba wao wanapokea rushwa. Wakakubaliana wote wawili waende [badala yake] kwa kuhani [mtabiri] wa Juhaynah awahukumie. Ikateremshwa Aayah: ((Je, huoni wale ambao wanadai kwamba …))

 

وَقِيلَ: نَزَلَتْ فِي رَجُلَيْنِ اِخْتَصَمَا، فَقَالَ أَحَدُهُمَا: نَتَرَافَعُ إِلَى النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) وَقَالَ الآخَرُ: إِلَى كَعْبِ بْنِ الأَشْرَفِ. ثُمَّ تَرَافَعَا إِلَى عُمَرَ فَذَكَرَ لَهُ أَحَدُهُمَا الْقِصَّةَ فَقَالَ لِلَّذِي لَمْ يَرْضَ بِرَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ) أَكَذَلِكَ؟ قَالَ نَعَمْ. فَضَرَبَهُ بِالسَّيْفِ فَقَتَلَهُ

Na imesemekana kwamba imeteremka kuhusu watu wawili waliokuwa na mgogoro. Akasema mmoja wao: “Tukapeleke mashitaka yetu kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).” Mwengine akasema: “Tupeleke kwa Ka’b bin Al-Ashraf” (Myahudi). Kisha wote wawili wakamwendea ‘Umar (رضي الله عنه) . Mmoja wao akamwelezea kadhia yao. ‘Umar akamuuliza ambaye hakuridhia kupeleka kesi yake kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Je, ni kweli alivyosema [mwenzako]?” Akajibu: “Ndio!”  Akampiga panga na akamuua.

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah An-Nisaa (4: 60) pamoja na masisitizo wa kuelewa maana ya Twaaghuwt.

 

2-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Baqarah (2: 11).

 

3-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-A’raaf (7: 56).

 

4-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Maai’dah (5: 50).

   

5-Maelezo ya Ash-Sha’biyy (رحمه الله) kuhusu sababu ya kuteremshwa Aayah (Suwrah An-Nisaa 4: 60).

 

6-Tofauti baina ya iymaan ya kweli na ya uongo.

 

7-Kisa cha ‘Umar (رضي الله عنه) na Mnafiki.

 

8-Hakuna anayepata iymaan isipokuwa mpaka hawaa zake zifuate na aliyokuja nayo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

 

Share