40-Kitaab At-Tawhiyd: Anayekanusha Chochote Kuhusu Majina Na Sifa Za Allaah

Mlango Wa 40

بَابٌ مَنْ جَحَدَ شَيْئًا مِنَ الْأَسْمَاءِ وَالصِّفَاتِ

Anayekanusha Chochote Kuhusu Majina Na Sifa Za Allaah


 

 

 قَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:

Kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

 وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَـٰنِ ۚ قُلْ هُوَ رَبِّي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ مَتَابِ ﴿٣٠﴾

((Nao wanamkufuru Ar-Rahmaan. Sema: “Yeye Ndiye Rabb wangu, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake natawakali na Kwake ni mahali pangu pa kurejea kutubu”)) [Ar-Ra’d (13: 30)]

 

وَفِي صَحِيحِ الْبُخَارِيِّ،  قَالَ عَلِيٌّ: حَدِّثُوا النَّاسَ بِمَا يَعْرِفُونَ، أَتُرِيدُونَ أَنْ يُكَذَّبَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ؟!

Na katika Swahiyh Al-Bukhaariy amesema ‘Aliyy(رضي الله عنه) : Wasemezeni watu kwa njia itakayowawezesha kufahamu kwa urahisi. Je mnataka Akadhibishwe Allaah na Rasuli Wake?!

 

وَرَوَى عَبْدُ الرَّزَّاقِ عَنْ مَعْمَرٍ، عَنِ ابْنِ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنَّهُ رَأَى رَجُلاً اِنْتَفَضَ لَمَّا سَمِعَ حَدِيثًا عَنِ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي الصِّفَاتِ، اِسْتِنْكَارًا لِذَلِكَ فَقَالَ: مَا فَرَقُ هَؤُلاءِ؟ يَجِدُونَ رِقَّةً عِنْدَ مُحْكَمِهِ وَيَهْلِكُونَ عِنْدَ مُتَشَابِهِهِ! -  اِنْتَهَى

Abdur-Razzaaq amesimulia kutoka kwa Ma’mar, kutoka kwa Ibn Twaawuws, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba: (Ibn ‘Abbaas) alimwona mtu akisimamisha miguu yake kwa kuchukiwa aliposikia Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Sifa za Allaah. Hapo (Ibn ‘Abbaas) akasema: Kitu gani kinachowatia uoga watu hawa? Wanachukia Aayah zilizo muhkam (waziwazi kabisa) na wanajiangamiza kwa Aayah za mutashaabihaat (Aayah zisizokuwa bayana kwao). 

 

 وَلَمَّا سَمِعَتْ قُرَيْشٌ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَذْكُرُ الرَّحْمَنَ أَنْكَرُوا ذَلِكَ فَأَنْزَلَ اللَّهُ فِيهِمْ: ((وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَـٰنِ ۚ ))  

Na Maquraysh walipomsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akimtaja Ar-Rahmaan walikanusha Sifa hiyo. Allaah Akawateremshia: ((Nao wanamkufuru Ar-Rahmaan …))

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Hana iymaan anayekanusha lolote katika Majina au Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى).

 

2-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Ar-Ra’d (13: 30).

 

3-Epuka kuzungumza katika namna ambayo msikilizaji hataelewa waziwazi

 

4-Kutajwa sababu zinazopelekea kumkanusha Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) hata kama bila kudhamiria.

 

5-Onyo la Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنه) kuwa yeyote anayekanusha Sifa yoyote ya Allaah (سبحانه وتعالى) ataangamia.

 

Share