49-Kitaab At-Tawhiyd: Kusema Mali Hii Ni Natija, Juhudi, Kazi, Elimu Yangu Kinyume Na Tawhiyd

Mlango Wa 49

باب:  وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ رَحْمَةً مِّنَّا مِن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ هَـٰذَا لِي

Kusema Kuwa Mali Hii Ni Natija Juhudi Kazi Na Elimu Yangu Ni Kinyume Na Tawhiyd


 

قَوْلُ اللَّهِ تَعَالَى:

Kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ رَحْمَةً مِّنَّا مِن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ هَـٰذَا لِي وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِن رُّجِعْتُ إِلَىٰ رَبِّي إِنَّ لِي عِندَهُ لَلْحُسْنَىٰ ۚ فَلَنُنَبِّئَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِمَا عَمِلُوا وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ ﴿٥٠﴾

((Na Tunapomuonjesha rahmah kutoka Kwetu baada ya dhara iliyomgusa, bila shaka husema: “Haya nayastahiki mimi na sidhani kama Saa ya Qiyaamah itasimama. Na nitakaporejeshwa kwa Rabb wangu hakika nitapata mazuri Kwake.” Basi bila shaka Tutawabainishia wale waliokufuru yale waliyoyatenda, na bila shaka Tutawaonjesha adhabu nzito)) [Fusw-swilat (41: 50)]

 

 قَالَ مُجَاهِدٌ: هَذَا بِعَمَلِي وَأَنَا مَحْقُوقٌ بِهِ

Mujaahid amesema: (kuhusu maana ya maneno: “haadhaa liy” inamaanisha): “Hii ni natija ya kazi yangu nami ndiye ninayeistahiki.”

 

وَقَالَ اِبْنُ عَبَّاسٍ: يُرِيدُ مِنْ عِنْدِي  

Na Ibn ‘Abbaas amesema: (inamaanisha): “Kilichokuwa kwangu”

 

وَقَوْلُهُ:  

Na kauli Yake:

قَالَ إِنَّمَا أُوتِيتُهُ عَلَىٰ عِلْمٍ عِندِي ۚ  

(([Qaaruwn] Akasema: “Hakika nimepewa haya kwa sababu ya elimu yangu”)) [Al-Qaswasw (28:78)]

 

قَالَ قَتَادَةُ: عَلَى عِلْمٍ مِنِّي بِوُجُوهِ الْمَكَاسِبِ.

Qataadah amesema: (katika kuifasiri Aayah hiyo): “Mali hii nimepewa mimi kwa sababu ya uhodari na uzoefu wangu katika kuchuma.”

 

وَقَالَ آخَرُونَ: عَلَى عِلْمٍ مِنَ اللَّهِ أَنِّي لَهُ أَهْلٌ، وَهَذَا مَعْنَى قَوْلِ مُجَاهِدٍ: أُوتِيتُهُ عَلَى شَرَفٍ.

Na Wanachuoni wengineo wamesema: (ina maana kwamba): “Kutokana na elimu kutoka kwa Allaah ambayo mimi khususan nimestahiki kutoka Kwake” Na hii ndio maana ya kauli ya Mujaahid: “Nimepewa hii (mali) kwa kutokana na sharafu yangu kuu.”

 

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((إِنَّ ثَلاثَةً مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَبْرَصَ وَأَقْرَعَ وَأَعْمَى، فَأَرَادَ اللَّهُ أَنَّ يَبْتَلِيَهُمْ، فَبَعَثَ إِلَيْهِمْ مَلَكًا. فَأَتَى الأَبْرَصَ فَقَالَ: أَيُّ شَيْءٍ أَحَبُّ إِلَيْكَ؟ قَالَ: لَوْنٌ حَسَنٌ وَجِلْدٌ حَسَنٌ وَيَذْهَبُ عَنِّي الَّذِي قَدْ قَذَرَنِي النَّاسُ بِهِ. قَالَ: فَمَسَحَهُ فَذَهَبَ عَنْهُ قَذَرَهُ، فَأُعْطِيَ لَوْنًا حَسَنًا وَجِلْدًا حَسَنًا. قَالَ: فَأَيُّ الْمَالِ أَحَبُّ إِلَيْكَ؟ قَالَ الإِبِلُ أَوْ الْبَقَرُ (شَكَّ إِسْحَاقُ) ، فَأُعْطِيَ نَاقَةً عُشَرَاءَ وَقَالَ بَارِكَ اللَّهُ لَكَ فِيهَا.

قَالَ: فَأَتَى الأَقْرَعَ فَقَالَ: أَيُّ شَيْءٍ أَحَبُّ إِلَيْكَ؟ قَالَ: شَعْرٌ حَسَنٌ  وَيَذْهَبُ عَنِّي الَّذِي قَدْ قَذَرَنِي النَّاسُ بِهِ. فَمَسَحَهُ فَذَهَبَ عَنْهُ وَأُعْطِيَ شَعْرًا حَسَنًا. فَقَالَ: أَيُّ الْمَالِ أَحَبُّ إِلَيْكَ؟ قَالَ: الْبَقَرُ أَوْ الإِبِلُ. فَأُعْطِيَ بَقَرَةً حَامِلاً،  قَالَ: بَارِكَ اللَّهُ لَكَ فِيهَا .

فَأَتَى الأَعْمَى فَقَالَ: أَيُّ شَيْءٍ أَحَبُّ إِلَيْكَ؟ قَالَ: أَنْ يَرُدَّ اللَّهُ إِلَيَّ بَصَرِي فَأُبْصِرُ بِهِ النَّاسَ، فَمَسَحَهُ فَرَدَّ اللَّهُ إِلَيْهِ بَصَرَهُ، قَالَ: فَأَيُّ الْمَالِ أَحَبُّ إِلَيْكَ؟ قَالَ: الْغَنَمُ، فَأُعْطِيَ شَاةً وَالِدًا، فَأُنْتَجَ هَذَانِ وَوَلَّدَ هَذَا فَكَانَ لِهَذَا وَادٍ مِنَ الإِبِلِ وَلِهَذَا وَادٍ مِنَ الْبَقَرِ وَلِهَذَا وَادٍ مِنَ الْغَنَمِ.

قَالَ: ثُمَّ إِنَّهُ أَتَى الأَبْرَصَ فِي صُورَتِهِ وَهَيْئَتِهِ فَقَالَ: رَجُلٌ مِسْكِينٌ وَابْنُ سَبِيلٍ قَدْ اِنْقَطَعَتْ بِيَ الْحِبَالُ فِي سَفَرِي، فَلا بَلاغَ لِيَ الْيَوْمَ إِلاَّ بِاللَّهِ ثُمَّ بِكَ، أَسْأَلُكَ بِالَّذِي أَعْطَاكَ اللَّوْنَ الْحَسَنَ وَالْجِلْدَ الْحَسَنَ وَالْمَالَ،  بَعِيرًا أَتَبَلَّغُ بِهِ فِي سَفَرِي، فَقَالَ: الْحُقُوقُ كَثِيرَةٌ. فَقَالَ لَهُ كَأَنِّي أَعْرِفُكَ! أَلَمْ تَكُنْ أَبْرَصَ يَقْذَرُكَ النَّاسُ، فَقِيرًا فَأَعْطَاكَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ الْمَالَ؟ فَقَالَ: إِنَّمَا وَرِثْتُ هَذَا الْمَالَ كَابِرًا عَنْ كَابِرٍ. فَقَالَ: إِنْ كُنْتَ كَاذِبًا فَصَيَّرَكَ اللَّهُ إِلَى مَا كُنْتَ.

قَالَ: ثُمَّ إِنَّهُ أَتَى الأَقْرَعَ فِي صُورَتِهِ فَقَالَ لَهُ مِثْلَ مَا قَالَ لِهَذَا، وَرَدَّ عَلَيْهِ مِثْلَ مَا رَدَّ عَلَيْهِ هَذَا، فَقَالَ إِنْ كُنْتَ كَاذِبًا فَصَيَّرَكَ اللَّهُ إِلَى مَا كُنْتَ.

 قَالَ "وَأَتَى الأَعْمَى فِي صُورَتِهِ فَقَالَ: رَجُلٌ مِسْكِينٌ وَابْنُ سَبِيلٍ قَدْ اِنْقَطَعَتْ بِيَ الْحِبَالُ فِي سَفَرِي، فَلا بَلاغَ لِيَ الْيَوْمَ إِلاَّ بِاللَّهِ ثُمَّ بِكَ، أَسْأَلُكَ بالَّذِي رَدَّ عَلَيْكَ بَصَرَكَ، شَاةً أَتَبَلَّغُ بِهَا فِي سَفَرِي. فَقَالَ قَدْ كُنْتُ أَعْمَى فَرَدَّ اللَّهُ إِلَيَّ بَصَرِي، فَخُذْ مَا شِئْتَ وَدَعْ مَا شِئْتَ فَوَاللَّهِ لاَ أَجْهَدُكَ الْيَوْمَ بِشَيْءٍ أَخَذْتَهُ لِلَّهِ. فَقَالَ: أَمْسِكْ مَالَكَ فَإِنَّمَا ابْتُلِيتُمْ،   فَقَدْ رَضِيَ اللَّهُ عَنْكَ وَسَخِطَ عَلَى صَاحِبَيْكَ))

Na Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah(رضي الله عنه)  kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah(صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Allaah alitaka kuwajaribu watu watatu katika wana wa Israaiyl; mkoma, kipofu na kipara Akawatumia Malaika. Akamwendea mkoma akamuuliza: “Kitu gani ukipendacho mno?” Akajibu: “Rangi na ngozi nzuri [ya mwili], na uniondokee [ukoma] niliokuwa nao unaowakera watu.” Akasema: [Malaika] Akamgusa ukamuondokea ugonjwa akapewa rangi na ngozi nzuri. Akamuuliza: “Mali ipi upendayo zaidi?” Akajibu: “Ngamia au ng’ombe.” [Msimuliaji Is-haaq hana uhakika ni yupi] Basi mwenye ukoma akapewa ngamia jike mwenye mimba. [Malaika] Akasema [kumuombea]: “Allaah Akubarikie navyo.”

Kisha Malaika akaenda kwa kipara akamuuliza: “Kitu gani ukipendacho mno?” Akajibu: “Nywele nzuri na kiniondokee [kipara] kinachowakera watu.” Akamgusa, kikamuondoka [kipara] akapewa nywele nzuri. Akamuuliza: “Mali ipi upendayo zaidi?” Akajibu: “Ng’ombe au ngamia.” Akapewa ng’ombe jike mwenye mimba. Akasema [kumuombea]: “Allaah Akubarikie navyo.”

Akamwendea kipofu: Akamuuliza: “Kitu gani ukipendacho mno?” Akajibu: “Allaah Anirudishie macho yangu nipate kuwaona watu.” Akamgusa, Allaah Akamrudishia macho yake. Akamuuliza: “Mali ipi uipendayo zaidi”? Akajibu: “Mbuzi.” Akapewa mbuzi mwenye mimba. Baada ya hapo, wanyama wote watatu wakazaa na kuzaliana hadi kwamba kila mmoja alikuwa na bonde la ngamia, na mwengine bonde la ng’ombe na mwengine bonde la mbuzi.

Akasema: Kisha [Malaika] akamrudia mkoma akiwa katika hali kama yake ya mtu mwenye ukoma. Akasema: “Mimi ni masikini, nimekatikiwa na nyenzo zangu safarini, kwa hiyo sina leo wa kunitimizia isipokuwa Allaah kisha wewe. Nakuomba kwa Ambaye Amekupa rangi na ngozi nzuri, na mali, unigawie ngamia ili anifikishe katika safari yangu.” Akajibu: “Nina majukumu mengi [kwa hiyo siwezi kukupa kitu!].” [Malaika] Akasema: “Kana kwamba nakujua? Si wewe uliyekuwa na ukoma wakikereka watu, na ulikuwa masikini kisha Allaah ‘Azza wa Jalla [Aliyetukuka na Utukufu] Akakupa mali [yote hii]?” Akajibu: “[Hapana ni uongo!] Hakika nimerithi yote hayo kwa mababu zangu.” [Malaika] akasema: “Ikiwa unasema uongo, basi Allaah Akurudishe kama ulivyokuwa awali.”

Akamwendea aliyenyonyoka nywele (kipara) akiwa katika hali kama yake ya mtu mwenye kipara. Akamuuliza kama alivyomuuliza huyu [mwenye ukoma], naye akamjibu kama alivyojibu naye. Akamwambia: Ikiwa unasema uongo, basi Allaah Akurudishe kama ulivyokuwa awali. 

Akasema: Akamwendea kipofu akiwa katika hali kama yake ya mtu kipofu. Akamwambia: “Mimi ni masikini na msafiri, nimekatikiwa na nyenzo zangu safarini, kwa hiyo sina leo wa kunitimizia isipokuwa Allaah kisha wewe. Nakuomba kwa Ambaye Amekupa macho yako, unigawie mbuzi ili anifikishe katika safari yangu.” Akajibu: “Bila shaka! Nilikuwa kipofu na Allaah Akanirudishia macho yangu [na nilikuwa masikini Allaah Akanitajirisha]. Chukua utakacho, na acha utakacho, kwani wa-Allaahi sitakuzuia chochote [unachohitaji] kuchukua kwa ajili ya Allaah.” Akasema [kumuombea]: “Weka mali yako, kwani hakika mmejaribiwa, na hakika Allaah Ameridhika nawe na Amewaghadhibikia wenzako”)) [Al-Bukhaariy na Muslim ]  

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Fus-Swilat (41: 50).

 

2-Maana ya: 

لَيَقُولَنَّ هَـٰذَا لِي

((Haya nayastahiki mimi)).

 

3-Maana ya:  

أُوتِيتُهُ عَلَىٰ عِلْمٍ عِندِي ۚ

((Nimepewa haya kwa sababu ya elimu yangu)).

 

4-Mafunzo makubwa katika kisa cha kusisimua.

 

 

 

Share