63-Kitaab At-Tawhiyd: Kulinda Ahadi Za Allaah Na Nabiy Wake

Mlango Wa 63

بَابٌ مَا جَاءَ فِي ذِمَّةِ اَللَّهِ وَذِمَّةِ نَبِيِّهِ

Kulinda Ahadi Za Allaah Na Nabiy Wake


 

 

وَقَوْلُهُ تَعَالَى:

Na kauli Yake Ta’aalaa:

 

وَأَوْفُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ إِذَا عَاهَدتُّمْ وَلَا تَنقُضُوا الْأَيْمَانَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ اللَّـهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ ﴿٩١﴾

((Na timizeni ahadi ya Allaah mnapoahidi, na wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha; na mmekwishamfanya Allaah kuwa ni Mdhamini wenu. Hakika Allaah Anajua yale mnayoyafanya)) [An-Nahl (16: 91)]  

 

عَنْ بُرَيْدَةَ قَالَ: كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) إِذَا أَمَّرَ أَمِيرًا عَلَى جَيْشٍ أَوْ سَرِيَّةٍ أَوْصَاهُ بِتَقْوَى اَللَّهِ - وَمَنْ مَعَهُ مِنَ الْمُسْلِمِينَ خَيْرًا. فَقَالَ: ((اُغْزُوَا بِسْمِ اَللَّهِ فِي سَبِيلِ اَللَّهِ ، قَاتِلُوا مَنْ كَفَرَ بِاَللَّهِ اُغْزُوَا ولاَ تَغُلُّوا وَلاَ تَغْدِرُوا وَلاَ تُمَثِّلُوا وَلاَ تَقْتُلُوا وَلِيدًا.

وَإِذَا لَقِيتَ عَدُوَّكَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ فَادْعُهُمْ إِلَى ثَلاثِ خِصَالٍ (أَوْ خِلالٍ)، فَأَيَّتُهُنَّ مَا أَجَابُوكَ فَاقْبَلْ مِنْهُمْ، وَكُفَّ عَنْهُمْ ثُمَّ اُدْعُهُمْ إِلَى الإِسْلامِ. فَإِنْ أَجَابُوكَ: فَاقْبَلْ مِنْهُمْ ثُمَّ اُدْعُهُمْ إِلَى اَلتَّحَوُّلِ مِنْ دَارِهِمْ إِلَى دَارِ الْمُهَاجِرِينَ وَأَخْبِرْهُمْ أَنَّهُمْ إِنْ فَعَلُوا ذَلِكَ فَلَهُمْ مَا لِلْمُهَاجِرِينَ، وَعَلَيْهِمْ مَا عَلَى الْمُهَاجِرِينَ، فَإِنْ أَبَوْا أَنْ يَتَحَوَّلُوا مِنْهَا فَأَخْبِرْهُمْ أَنَّهُمْ يَكُونُونَ كَأَعْرَابِ الْمُسْلِمِينَ يَجْرِي عَلَيْهِمْ حُكْمُ اَللَّهِ تَعَالَى وَلاَ يَكُونُ لَهُمْ فِي الْغَنِيمَةِ وَالْفَيءِ شَيءٌ إِلاَّ أَنْ يُجَاهِدُوا مَعَ الْمُسْلِمِينَ، فَإِنْ هُمْ أَبَوْا، فَاسْأَلْهُمْ الْجِزْيَةَ، فَإِنْ هُمْ أَجَابُوكَ فَاقْبَلْ مِنْهُمْ، وَكُفَّ عَنْهُمْ، فَإِنْ هُمْ أَبَوْا، فَاسْتَعِنْ بِاَللَّهِ وَقَاتِلْهُم.

وَإِذَا حَاصَرْتَ أَهْلَ حِصْنٍ فَأَرَادُوكَ أَنْ تَجْعَلَ لَهُمْ ذِمَّةَ اَللَّهِ وَذِمَّةَ نَبِيِّهِ، فَلا تَجْعَلْ لَهُمْ ذِمَّةَ اَللَّهِ وَذِمَّةَ نَبِيِّهِ، وَلَكِنِ اِجْعَلْ لَهُمْ ذِمَّتَكَ وَذِمَّةَ أَصْحَابِكَ، فَإِنَّكُمْ أَنْ تَخْفِرُوا ذِمَمَكُمْ وَذِمَّةَ أَصْحَابِكُمْ أَهْوَنُ مِنْ أَنْ تَخْفِرُوا ذِمَّةَ اَللَّهِ وَذِمَّةَ نَبِيِّهِ.

 وَإِذَا حَاصَرْتَ أَهْلَ حِصْنٍ فَأَرَادُوكَ أَنْ تُنْزِلَهُمْ عَلَى حُكْمِ اَللَّهِ، فَلا تُنْزِلْهُمْ عَلَى حُكْمِ اَللَّهِ وَلَكِنْ أَنْزِلْهُمْ عَلَى حُكْمِكَ فَإِنَّكَ لاَ تَدْرِي أَتُصِيبُ فِيهِمْ حُكْمَ اَللَّهِ أَمْ لاَ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Imepokelewa kutoka kwa Buraydah (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapomwakilisha uongozi amiri wa jeshi au kikosi, alimuusia kumcha Allaah na kuwafanyia wema Waislamu waliokuwa naye. Alikuwa akisema: ((Anzeni kupigana vita kwa BismiLLaah, katika njia ya Allaah. Piganeni na wanaomkanusha Allaah. Piganeni vita na msichukue ngawira kwa njia isiyostahiki, na msivunje mkataba wala msikate viungo vya maiti, wala kuua watoto.

 

Mnapokutana na maadui washirikina, walinganieni mambo matatu.   Wakikubali mojawapo basi wakubalini kwa ahadi yao wala msiendelee kupigana. Kisha waiteni katika Uislamu. Wakisilimu waombeni wahamie katika miji ya Muhaajirina (ya Kiislamu). Waambieni kwamba wakifanya hivyo, basi watastahiki haki zote za Muhaajirina. Wakikataa kuhama, basi watakuwa kama Mabedui Waislamu na kwamba [hawatokuwa huru bali] watanyenyekea amri za Allaah (سبحانه وتعالى) kama Waislamu wengine, lakini hawatopata ngawira yoyote mpaka wapigane bega kwa bega na Waislamu. Wakikataa [kusilimu] basi watalazimika kulipa jizyah[1].  Wakikubali basi acheni kupigana nao. Lakini wakikataa [kulipa jizyah] basi takeni msaada kwa Allaah na piganeni nao.

 

Mkizingira ngome na waliozingirwa wakikuombeni hifadhi na ulinzi kwa Jina la Allaah na Rasuli Wake, msiwape dhamana ya Allaah na Rasuli Wake, bali wapeni dhamana kwa niaba yako na wenzako kwani itakuwa ni dhambi ndogo pale isipoheshimiwa dhamana utakayoitoa wewe na wenzako kuliko kutokuheshimu dhamana ya Jina la Allaah na Rasuli Wake. Mkizingira ngome na waliozingirwa wanawatakeni muwaachie watoke kwa mujibu wa hukmu ya Allaah, msiwaachie kwa mujibu ya hukmu ya Allaah, bali   watoeni kwa hukmu yako, kwani hujui kama utaweza au hatoweza kufuata hukmu ya Allaah juu yao)) [Muslim]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tofauti baina hifadhi ya Allaah (سبحانه وتعالى) na ya Rasuli Wake  

  (صلى الله عليه وآله وسلم) na hifadhi ya Waislamu.

 

2-Maelekezo ya kuchagua lenye khatari ndogo.

 

3-Amri ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Anzeni kupigana vita kwa BismiLLaah, katika njia ya Allaah)).

 

4-Amri ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Piganeni na wanaomkanusha  Allaah)).

 

5-Amri ya Nabiy: ((Takeni msaada kwa Allaah na piganeni nao)).

 

6-Kuna tofauti baina ya amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) na ya 'Ulamaa.

 

7-Hukmu ya Swahaba huenda isilingane na hukmu Allaah (سبحانه وتعالى).

 

 

 

 

 

 

 

 

 

[1] Kodi wanayotozwa wasio Waislamu ya ulinzi katika serikali ya Kiislamu.

Share