65-Kitaab At-Tawhiyd: Haiombwi Shafaa-ah Ya Allaah Juu Ya Viumbe Vyake

Mlango Wa 65

بَابٌ لَا يُسْتَشْفَعُ بِاَللَّهِ عَلَى خَلْقِهِ

Haiombwi Shafaa-ah Ya Allaah Juu Ya Viumbe Vyake


 

 

عَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ : جَاءَ أَعْرَابِيٌّ إِلَى اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! نُهِكَتِ الأَنْفُسُ وَجَاعَ الْعِيَالُ وَهَلَكَتِ الأَمْوَالُ فَاسْتَسْقِ لَنَا رَبَّكَ، فَإِنَّا نَسْتَشْفِعُ بِاَللَّهِ عَلَيْكَ، وَبِكَ عَلَى اَللَّهِ. فَقَالَ اَلنَّبِيُّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((سُبْحَانَ اَللَّهِ! سُبْحَانَ اَللَّهِ!)) فَمَا زَالَ يُسَبِّحُ حَتَّى عُرِفَ ذَلِكَ فِي وُجُوهِ أَصْحَابِهِ ثُمَّ قَالَ: ((وَيْحَكَ! أَتَدْرِي مَا اَللَّهُ؟ إِنَّ شَأْنَ اَللَّهِ أَعْظَمُ مِنْ ذَلِكَ، إِنَّهُ لاَ يُسْتَشْفَعُ بِاَللَّهِ عَلَى أَحَدٍ مِنْ خَلْقِهِ)) وَذَكَرَ الْحَدِيثَ رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ

Imepokelewa kutoka kwa Jubayr bin Mutw’-im(رضي الله عنه)  amesema: Alikuja Bedui kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Watu wanaangamia, na watoto wana njaa, mali imeangamia [mimea na wanyama], basi muombe Rabb wako Atuletee mvua, kwani tunaomba shafaa’ah ya Allaah kwako na shafaa’ah yako kwa Allaah.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Subhaana-Allaah! Subhaana Allaah!)). Akaendelea kumtakasa Allaah mpaka athari yake ikadhihiri nyusoni mwa Maswahaba. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Ole wako! Unamjua nani Allaah? Hakika Utukufu wa Allaah ni adhimu zaidi kuliko hilo! Haiombwi shafaa’ah ya Allaah juu ya yeyote kati ya viumbe Wake)) [Akataja Hadiyth Abuu Daawuwd]      

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

 

1-Nabiy kukaripia kunaposemwa: “Tunaomba shafaa’ah ya Allaah kwako.”

 

2-Ghadhabu ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ilidhihirika kwa Maswahaba  (رضي الله عنهم).

 

3-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakukemea ombi la shafaa’ah yake kwa Allaah.

 

4-Maana ya Subhana-Allaah. (Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko juu kabisa ya viumbe Vyake na Ametakasika kabisa dhidi ya ila na hahitaji lolote].

 

5-Waislamu walimuomba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aombe mvua.

 

 

Share