042-Aayah Na Mafunzo: Sifa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Katika Tawraat

Aayah Na Mafunzo:

Al-Baqarah

Sifa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Katika Tawraat

 

 

وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na wala msichanganye haki kwa batili na mkaficha haki; na hali mnajua

 

Mafunzo:

Atwaa bin Yaasir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba: Nilikutana na ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  nikasema: Nielezee sifa za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zilizopo katika Tawraat. Akasema: Sawa. Wa-Allaahi hakika amesifiwa kwenye Tawraat kwa baadhi ya sifa katika Qur-aan. Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi na mbashiriaji na mwonyaji na ngao ya Waumini. Wewe ni mja na Rasuli Wangu. Na nikakuita mwenye kutawakkal. Yeye si mwenye maneno makali wala si msusuwavu, wala hazui ovu kwa ovu, wala halipizi uovu kwa uovu lakini anasamehe na kuachilia mbali. Na Allaah Hatomfisha mpaka asimamishe mila iliyojikunja kwa kusema: Laa ilaaha illa Allaah [hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah] na afungue kwayo macho yaliyopofuka, na masikio yasiyosikia, na nyoyo zilizofungwa. [Al-Bukhaariy (2125)]. 

 

Share