116-Aayah Na Mafunzo: Kumsingizia Allaah Subhanaahu Wa Ta’aalaa Kuwa Ana Mwana Ni Kumshutumu Allaah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kumsingizia Allaah Subhanaahu Wa Ta’aalaa Kuwa Ana Mwana Ni Kumshutumu Allaah

 

 

وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾

116. Na wakasema: “Allaah Amejichukulia mwana.” Subhaanah! Utakasifu ni Wake. Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii.

 

 

Mafunzo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (قَالَ اللَّهُ: كَذَّبَنِي ابْنُ آدَمَ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، وَشَتَمَنِي وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، أَمَّا تَكْذِيبُهُ إِيَّاىَ أَنْ يَقُولَ إِنِّي لَنْ أُعِيدَهُ كَمَا بَدَأْتُهُ، وَأَمَّا شَتْمُهُ إِيَّاىَ أَنْ يَقُولَ اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا، وَأَنَا الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ أَلِدْ وَلَمْ أُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لِي كُفُؤًا أَحَدٌ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah  (رضي الله عنهما)amesema:  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Allaah Amesema: Mwana Aadam amenikadhibisha, wala hapaswi hilo! Na amenishutumu mja wangu na wala hapaswi hilo! Ama kunikadhibisha kwake, amedai kuwa Sitoweza kumrudisha (kumfufua) kama alivyokuwa. Ama kunishutumu, ni kudai kuwa Nina mwana na ilhali   Mimi ni Asw-Swamad (Aliyekamilika sifa za utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote) Ambaye Sikuzaa wala Sikuzaliwa na hakuna chochote kinachofanana na kulingana Nami.”   [Al-Bukhaariy]

 

 

Share