155-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Dhikru Ya Istirjaa'

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Fadhila Za Dhikru Ya Istirjaa’

(Hakika sisi ni wa Allaah, na hakika sisi Kwake wenye kurejea)

 

www.alhidaaya.com

 

 

وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾

155. Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri.

 

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿١٥٦﴾

156. Wale ambao unapowafika msiba husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.”

 

أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ﴿١٥٧﴾

 

Mafunzo:

 

Muislamu apatapo msiba au janga lolote lile ikiwa ni kufiwa, maradhi, kupata khasara katika mali, mateso, maafa ya aina yoyote n.k. basi hapo hapo aombe du’aa hii:

 

إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ, اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا

 

 

Dalili ni Hadiyth ya Ummuu Salamaah (رضي الله عنها) ambaye amehadithia:  Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Hakuna Muislamu anayefikwa na msiba akasema Alivyoamrishwa na Allaah: (Hakika sisi ni wa Allaah, na hakika sisi Kwake wenye kurejea, ee Allaah, nilipe kwa msiba wangu na nipe badala yake kilicho bora kuliko huo [msiba]), basi hakuna ila Allaah Atampa kilicho bora kuliko (msiba huo).” Abuu Salamah alipofariki nilisema: Muislamu gani ni bora kuliko Abuu Salamah ambaye familia yake ilikuwa ya kwanza kuhajiri kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?. Kisha nikasema (du’aa hiyo) na Allaah Akanipa Rasulu-Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) badala yake…. [Muslim (910)]

 

 

Share