214-Aayah Na Mafunzo: Kuipata Jannah Si Wepesi Inahitaji Juhudi Ya ‘Amali Na Kujizuia Maasi

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kuipata Jannah Si Wepesi Inahitaji Juhudi Ya ‘Amali Na Kujizuia Maasi

 

  www.alhidaaya.com

 

 

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّـهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّـهِ قَرِيبٌ ﴿٢١٤﴾

214. Je, mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali bado haijakufikieni (mitihani) kama ya wale waliopita kabla yenu? Iliwagusa dhiki za umasikini na maafa ya magonjwa na njaa na wakatetemeshwa mpaka Rasuli na wale walioamini pamoja naye wanasema: “Lini itafika nusura ya Allaah?” Tanabahi! Hakika nusura ya Allaah iko karibu.

 

 

Mafunzo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لَمَّا خَلَقَ اللَّهُ الْجَنَّةَ وَالنَّارَ أَرْسَلَ جِبْرِيلَ إِلَى الْجَنَّةِ فَقَال: انْظُرْ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  قَالَ:  فَجَاءَهَا وَنَظَرَ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعَدَّ اللَّهُ لِأَهْلِهَا فِيهَا.  قَالَ:  فَرَجَعَ إِلَيْهِ قَالَ: فَوَعِزَّتِكَ لَا يَسْمَعُ بِهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا، فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ بِالْمَكَارِهِ، فَقَالَ: ارْجِعْ إِلَيْهَا فَانْظُرْ إِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  قَالَ: فَرَجَعَ إِلَيْهَا فَإِذَا هِيَ قَدْ حُفَّتْ بِالْمَكَارِهِ،  فَرَجَعَ إِلَيْهِ فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ خِفْتُ أَنْ لَا يَدْخُلَهَا أَحَدٌ. قَالَ: اذْهَبْ إِلَى النَّارِ فَانْظُرْ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  فَإِذَا هِيَ يَرْكَبُ بَعْضُهَا بَعْضًا،  فَرَجَعَ إِلَيْهِ فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَا يَسْمَعُ بِهَا أَحَدٌ فَيَدْخُلَهَا، فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ بِالشَّهَوَاتِ فَقَالَ: ارْجِعْ إِلَيْهَا فَرَجَعَ إِلَيْهَا فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ خَشِيتُ أَنْ لَا يَنْجُوَ مِنْهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا)) الترمذي و قال حديث حسن صحيح – ابو داود والنسائي

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Alipoumba Jannah na moto, Alimtuma Jibriyl Jannah Akimwambia: Iangalie na angalia matayarisho Niliyoyaandaa  kwa ajili ya wakazi wake. Akasema: Kwa hivyo alikuja kuiangalia na kuangalia maandalizi Aliyoyaandaa Allaah kwa ajili ya wakazi Wake. Akasema: Akarejea kwa Allaah na kusema: Naapa kwa Utukufu Wako, hakuna atakayesikia (habari yake) ila tu ataingia (Jannah). Kisha Akaamrisha izungushwe mambo magumu watu wasiyoyapenda, Akasema: Rejea na angalia yale Niliyoyaandaa kwa ajili ya wakazi wake. Akasema: Kisha akarejea na akakuta imezungukwa na mambo magumu watu wasiyoyapenda. Hapo alirejea kwa Allaah na akasema: Naapa kwa Utukufu Wako, nina khofu hakuna hata mtu mmoja atakayeingia. Akasema: Nenda motoni ukauangalie na uangalie Niliyoyaandaa kwa ajili ya wakazi wake. Akaona ulikuwa na matabaka moja juu ya tabaka jingine. Akarejea kwa Allaah na akasema: Naapa kwa Utukufu Wako hakuna hata mmoja ausikiae (sifa zake) atakayeingia. Kisha Allaah Aliamrisha Uhusishwe na matamanio ya nafsi). Kisha Allaah Akamuambia: Rejea tena (motoni). Alirejea tena na akasema: Naapa kwa Utukufu, wako nakhofia kuwa hapatokuwa na yeyote atakayenusurika nao)) [At-Tirmidhiy, akasema ni Hadiyth Hasan, na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy]

 

 

Share