252-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Fadhila Za Nabiy Ni Kupewa Mambo Matano

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Miongoni Mwa Fadhila Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Ni Kupewa Mambo Matano Ambayo Hakupewa Nabiy Yeyote

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa):

 

تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٢٥٢﴾

252. Hizo ni Aayaat za Allaah Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Rusuli.

 

 

Mafunzo:

 

عن جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أُعْطِيتُ خَمْسًا لَمْ يُعْطَهُنَّ أَحَدٌ قَبْلِي،  نُصِرْتُ بِالرُّعْبِ مَسِيرَةَ شَهْرٍ، وَجُعِلَتْ لِيَ الأَرْضُ مَسْجِدًا وَطَهُورًا، فَأَيُّمَا رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي أَدْرَكَتْهُ الصَّلاَةُ فَلْيُصَلِّ، وَأُحِلَّتْ لِيَ الْمَغَانِمُ وَلَمْ تَحِلَّ لأَحَدٍ قَبْلِي، وَأُعْطِيتُ الشَّفَاعَةَ، وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً، وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ عَامَّةً))

Jaabir bin Abdillah amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nimepewa mambo matano hakupewa yoyote kabla yangu; Nimenusuriwa na (kutiwa) kiwewe (nyoyoni mwa maadui) kwa mwendo wa mwezi. Na nimefanyiwa ardhi kuwa sehemu ya kufanyia ‘ibaadah na kujitwaharishia, basi mtu mtu yeyote katika ummah wangu akifikiwa na Swalaah, aswali. Na nimehalalishiwa ngawira hazikuwa halali kwa yeyote kabla yangu. Na nimepewa shafaa’ah (maombezi Siku ya Qiyaamah). Na alikuwa Nabiy akitumwa kwa watu wake pekee, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.” [Al-Bukhaariy (5011)]  

 

 

 

Share