254-Aayah Na Mafunzo: Kukimbilia Kutoa Swadaqah Kabla Ya Kufariki

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kukimbilia Kutoa Swadaqah Kabla Ya Kufariki

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa:)

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ ۗ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٥٤﴾

254. Enyi walioamini! Toeni katika Tulivyokuruzukuni kabla haijafika Siku ambayo hakutokuweko mapatano humo wala urafiki wala uombezi. Na makafiri wao ndio madhalimu.

 

 

Mafunzo:

 

عن أبي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم) فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ, أَيُّ الصَّدَقَةِ أَعْظَمُ أَجْرًا؟ قَالَ: ((أَنْ تَصَدَّقَ وَأَنْتَ صَحِيحٌ شَحِيحٌ تَخْشَى الْفَقْرَ وَتَأْمُلُ الْغِنَى وَلاَ تُمْهِلُ حَتَّى إِذَا بَلَغَتْ الْحُلْقُومَ قُلْتَ لِفُلاَنٍ كَذَا وَلِفلاَنٍ كَذَا وَقَدْ كَانَ لِفُلاَنٍ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  amesema: “Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Ni sadaka ipi yenye ujira mkubwa zaidi?  Akasema: ((Ni utoe swadaqah nawe umzima, unataka mali bado, unakhofia ufukara na unatarajia utajiri. Wala usichelewe mpaka roho ikafika kwenye koo, ukaanza kusema: fulani ana haki kadhaa na fulani ana haki kadhaa na fulani alikuwa ana haki kadhaa)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):

 

وَأَنفِقُوا مِن مَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَا أَخَّرْتَنِي إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ الصَّالِحِينَ﴿١٠﴾

Na toeni katika yale Tuliyokuruzukuni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti akasema: “Rabb wangu! Lau Ungeliniakhirisha mpaka muda wa karibu hivi, basi ningetoa swadaqah na ningelikuwa miongoni mwa Swalihina.” [Al-Munaafiquwn: 10]

 

 

 

 

 

Share