261-Aayah Na Mafunzo: Kutoa Mali Kwa Ajili Ya Allaah Ni Kuzidishiwa Mara Mia Saba

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Kutoa Mali Kwa Ajili Ya  Allaah Ni Kuzidishiwa Mara Mia Saba

 

www.alhidaaya.com

 

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

مَّثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّائَةُ حَبَّةٍ ۗ وَاللَّـهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦١﴾ 

261. Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja ya mbegu iliyotoa mashuke saba, katika kila shuke kuna punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye; na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.

 

Mafunzo:

 

Faida: Thawabu za kutoa kwa ajili ya Allaah: Aayaah kadhaa na Hadiyth zimetaja fadhila za kutoa mfano wa Hadiyth ni: ‘Uqbah bin ‘Amru bin Tha’alabah Abuu Mas‘uwd (رضي الله عنه) amehadithia kuwa mtu alitoa ngamia na hatamu yake kwa ajili ya Allaah, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Siku ya Qiyaamah utakuwa na ngamia mia saba pamoja na hatamu zao.” [Swahiyh An-Nasaaiy (3187)]

 

Pia: Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kutoa swadaqah hakupunguzi mali, Allaah Hamzidishii mja msamaha ila Humpa utukufu, na yeyote anayenyenyekea kwa ajili ya Allaah, Allaah Aliyetukuka Atampandisha Daraja.” [Muslim] 

 

 

Share