104-Aayah Na Mafunzo: Umuhimu Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Umuhimu Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu

Alhidaaya.com

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفلِحُونَ ﴿١٠٤﴾

Na watokeze kutoka kwenu umati wa watu unaolingania kheri na unaoamrisha mema na unaokataza munkari. Na hao ndio waliofaulu. [Aal-'Imraan: 104]

 

Mafunzo:

 

Umuhimu Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu:

 

Kuamrisha mema na kukataza maovu imesisitizwa katika Aayah kadhaa za Qur-aan na pia katika Sunnah imesisitzwa mno. Miongoni mwazo ni Hadiyth zifuatazo:

 

Hudhayfah bin Al-Yamaani (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake! Mtaamrisha mema na mtakataza maovu au sivyo Allaah Atakuleteeni adhabu kutoka Kwake, kisha mtamuomba wala Hatokuitikieni.” [Ahmad na At-Tirmidhy - Swahiyh At-Tirmdhiy (2169), Swahiyh Al-Jaami’ (7070)]

 

Pia: Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Atakayeona munkari (uovu) basi aubadilishe kwa mkono wake, na asipoweza basi kwa ulimi wake, na asipoweza basi kwa moyo wake (achukizwe) na huo ni udhaifu wa Iymaan.”  [Muslim]

 

 

 

Share