143-Aayah Na Mafunzo: Mdhabidhabina Ni Mtu Muovu Kabisa Ni Mwenye Nyuso Mbili

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Mdhabidhabina Mtu Muovu Kabisa Ni Mwenye Nyuso Mbili  

 

 

 

 

 مُّذَبْذَبِينَ بَيْنَ ذَٰلِكَ لَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ وَلَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿١٤٣﴾

143. Madhabidhabina baina ya hayo (iymaan na kufru), huku hawako wala huko hawako. Na ambaye Allaah Amempotoa huwezi kumpatia njia (ya kumwongoa).

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mtawakuta watu wana asili wanaonasibika nazo (wa jinsia tofauti tofauti na asili tofauti tofauti); wabora wao katika ujaahiliyyah ndio wabora wao katika Uislamu watakapokuwa na ‘ilmu ya shariy’ah za Dini. Na mtamkuta mbora wa watu katika jambo hili (la uongozi) ni mwenye kulichukia mno, na mtamkuta muovu wa watu ni mwenye nyuso mbili, ambaye anawaendea hawa kwa uso huu, na anawaendea wale kwa uso mwingine.” [Al-Bukhaariy na Muslim]. 

 

 

Share