027-Aayah Na Mafunzo: Tahadharisho La Kuazimia Kuua Au Kuuana

 

Aayah Na Mafunzo

Al-Maaidah

Tahadharisho La Kuazimia Kuua Au Kuuana

 

Alhidaaya.com

 

 

 

وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الْآخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّـهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ ﴿٢٧﴾

Na wasomee khabari ya wana wawili wa Aadam kwa haki walipotoa dhabihu ya kafara, ikakubaliwa ya mmoja wao lakini ya mwengine haikukubaliwa. (Asiyekubaliwa) akasema: Nitakuua tu!  (Aliyekubaliwa) akasema: Hakika Allaah Anatakabalia wenye taqwa. [Al-Maaidah: 27]

 

Mafunzo:

 

Tahadharisho la kuazimia kuua au kuuana: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Waislamu wawili watakapokabiliana kwa panga zao, basi wote wawili; muuaji na aliyeuliwa wataingia motoni.” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

 

Share