101-Aayah Na Mafunzo: Msiyadadisi Mambo Ambayo Allaah Amenyamazia

Aayah Na Mafunzo

Al-Maaidah

Msiyadadisi Mambo Ambayo Allaah Amenyamazia

Alhidaaya.com

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهَا ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٠١﴾

Enyi walioamini! Msiulizie mambo ambayo mkifichuliwa yatakuchukizeni. Na mkiyaulizia pale inapoteremshwa Qur-aan mtafichuliwa. Allaah Ameyasamehe hayo. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mvumilivu.

 

 

قَدْ سَأَلَهَا قَوْمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ثُمَّ أَصْبَحُوا بِهَا كَافِرِينَ ﴿١٠٢﴾

Walikwishayauliza hayo watu wa kabla yenu, kisha kutokana nayo, wakawa makafiri. [Al-Maaidah: 101-102]

 

 

Mafunzo:

 

Abuu Tha’labah Al-Khushaniy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah تعالى Amefaridhisha mambo ya Dini kwa hivyo msiyapuuze. Akaweka mipaka basi msiivuke, na Amekataza baadhi ya mambo kwa hivyo msiyafanye, na yale ambayo Amenyamazia ni kwa ajili ya rahmah Zake kwenu, si kwamba Ameyasahau kwa hivyo msiyadadisi.” [Ad-Daaraqutwniy na wengineo; Hadiyth Hasan].

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:

 

101-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Maaidah Aayah 101: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ

 

 

 

 

Share