186-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 186: لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan  186-Bila shaka mtajaribiwa katika mali zenu na nafsi zenu na bila shaka mtasikia

 

 

لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا أَذًى كَثِيرًا ۚ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ ﴿١٨٦﴾

186. Bila shaka mtajaribiwa katika mali zenu na nafsi zenu; na bila shaka mtasikia kutoka kwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na kutoka kwa wale walioshirikisha udhia mwingi. Lakini mkisubiri na mkawa na taqwa basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka ikibainisha mabaya aliyokuwa akiyafanya Myahudi Ka’b bin Al-Ashraf.    Alikuwa akimshambulia mno Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na anawashajiisha makafiri wa ki-Quraysh kumfanyia uadui Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).  Mayahudi wengine walikuwa pia wakimuudhi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na Swahaba zake.  Kisha Allaah Akamuamrisha Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) awasamehe na awapuuze Mayahudi hao. Ndipo hapo ikateremka Aayah hii. [Ka’b Ibn Maalik (رضي الله عنه)  ameipokea Abuu Daawuwd]

 

 

 

 

Share