123-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 123: لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa    123-Si kwa matamanio yenu wala si matamanio ya Watu wa Kitabu.

لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٢٣﴾

Si kwa matamanio yenu wala kwa matamanio ya Watu wa Kitabu. Atakayefanya uovu atalipwa kwalo, na wala hatopata mlinzi wala mwenye kumnusuru isipokuwa Allaah. (4:123)

Sababun-Nuzuwl:

Al-‘Awfiy amehadithia kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alisema kuhusu Aayah hii:

لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٢٣﴾

Si kwa matamanio yenu wala kwa matamanio ya Watu wa Kitabu. Atakayefanya uovu atalipwa kwalo, na wala hatopata mlinzi wala mwenye kumnusuru isipokuwa Allaah. (4:123)

Watu wa Dini mbali mbali walibishana. Watu wa Tawraat walisema: “Kitabu chetu ni Kitabu bora kabisa na Nabiy wetu (Muwsaa  عليه السلام) ni Nabiy bora kabisa.” Watu wa Injiyl wakasema kama hivyo. Waislamu wakasema: “Hakuna Dini isipokuwa ya Kiislamu, Kitabu chetu kimefuta vitabu vyote vingine na Nabiy wetu ni Nabiy wa mwisho na nyinyi mmeamrishwa katika vitabu vyenu kuamini na kufuata Kitabu chetu.” Hapo Allaah Akateremsha Aayah hii:

لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٢٣﴾

Si kwa matamanio yenu wala kwa matamanio ya Watu wa Kitabu. Atakayefanya uovu atalipwa kwalo, na wala hatopata mlinzi wala mwenye kumnusuru isipokuwa Allaah. (4:123)

 [Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

Share