042-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Maaidah Aayah 042: سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ أَكَّالُونَ لِلسُّحْتِ ۚ فَإِن جَاءُوكَ فَاحْكُم بَيْنَهُمْ أَوْ أَعْرِضْ عَنْهُمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Maaidah  042-(Hao ni) wenye kusikiliza kwa makini uongo, walaji haramu kwa pupa

 

سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ أَكَّالُونَ لِلسُّحْتِ ۚ فَإِن جَاءُوكَ فَاحْكُم بَيْنَهُمْ أَوْ أَعْرِضْ عَنْهُمْ ۖ وَإِن تُعْرِضْ عَنْهُمْ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيْئًا ۖ وَإِنْ حَكَمْتَ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٤٢﴾

(Hao ni) wenye kusikiliza kwa makini uongo, walaji haramu kwa pupa. Basi wakikujia wahukumu baina yao au wapuuze. Na ukiwapuuza, hawatowe za kukudhuru chochote. Na kama ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Allaah Anapenda wafanyao uadilifu. (5:42).

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kwamba: Walikuweko Quraydhwah na An-Nadhwiyr (makabila ya Mayahudi Madiynah). An-Nadhwiyr walikuwa wenye hadhi zaidi kuliko Quraydhwah. Ikawa pale mtu wa Quraydhwah anapoua mtu wa An-Nadhwiyr, huuliwa, lakini inapokuwa mtu wa An-Nadhwiyr ameua mtu wa Quraydhwah huitwa akapigwa mikaanga mia ya mitende kama diya. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotumwa kuwa ni Rasuli, mtu mmoja wa An-Nadhwiyr alimuua mtu wa Quraydhwah wakasema: Mleteni kwetu tumuue! Wakajibu: Sasa baina yetu na yenu yupo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) basi mleteni (atuhukumu)! Hapo ikateremka:

 

وَإِنْ حَكَمْتَ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٤٢﴾

 Na kama ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Allaah Anapenda wafanyao uadilifu. (5:42).

 

Na uadilifu ni (kisasi cha) nafsi kwa nafsi. Kisha ikateremka:

 

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿٥٠﴾

Je, wanataka hukumu za kijahiliya? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini. (5:50).

 

[Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan na wengineo]

 

Ibn Kathiyr amesema: Inaweza kuwa zimejumuika sababu mbili hizi (5:41-42) kwa wakati mmoja zikateremka Aayaat hizo kuhusu hayo, na Allaah Mjuzi zaidi

 

Share