Mwanzo Wa Maumbile - Kabla Ya Kuumbwa Ardhi Na Mbingu
Imeandikwa na Alhidaaya.com
Kabla ya kuanza visa vya Mitume na tuanze na utangulizi katika kujua hali ilivyokuwa kabla ya kuumbwa ardhi na mbingu. Zifuatazo ni Aya na Hadithi zinazothibitisha maumbile ya mwanzo kabisa.
Anasema Allaah سبحانه وتعالى
}}اللَّهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ{{
{{Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, na Yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu}} Az-Zumar: 62
Amesema vile vile
}}خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأََرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ الرَّحْمَانُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا{{
{{Ambaye ameziumba mbingu na ardhi, na viliomo ndani yake kwa siku sita. Kisha akatawala juu ya A'rshi, Arrahman, Mwingi wa Rehema! Uliza khabari zake kwa wamjuaye}} Al-Furqaan: 59
Ama Yeye Allaah سبحانه وتعالى ni wa mwanzo na wa milele na hakuna kilichokuwepo kabla Yake.
}}هُوَ الأََوَّلُ وَالأَخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ{{
{{Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhaahiri na wa Siri, naye ndiye Mjuzi wa kila kitu}} Al-Hadiid:3
Hadithi inatuelezea alipokuwa Allaah سبحانه وتعالى kabla ya kuumba ardhi na mbingu.
((عن عامر العقيلي أنه قال يا رسول الله أين كان ربنا قبل أن يخلق السموات والأرض قال كان في عماء ما فوقه هواء وما تحته هواء ثم خلق عرشه على الماء)) الإمام أحمد
(( Imetoka kwa 'Amir Al-'Aqiyliy kwamba alimuuliza Mtume صلى الله عليه وسلم Ewe Mjumbe wa Allaah, alikuwa wapi Mola wetu kabla ya kuumba mbingu na ardhi? Akasema: Alikuwa katika sehemu tupu (empty space) juu yake hewa na chini yake hewa kisha akaumba 'Arshi katika maji )) Imaam Ahmad
Na kabla ya kuumba chochote kwanza Allaah سبحانه وتعالى kwa Ujuzi Wake Aliiumba kalamu na Akaiamrisha hiyo kalamu iandike katika ubao wa 'Lawhun Mahfuudh" makadirio ya kila kitu.
((عن عبادة بن الصامت رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم إن أول ما خلق الله القلم ثم قال له اكتب فجرى في تلك الساعة بما هو كائن إلى يوم القيامة)) رواه الإمام أحمد وأبو داود والترمذي
((Kutoka kwa 'Ubaadah bin As-Swamit رضي الله عنه alisema; kasema Mtume صلى الله عليه وسلم kitu cha mwanzo kabisa alichokiumba Allaah سبحانه وتعالى ni kalamu kisha akaiamrisha iandike, ikaanza kuandika tokea saa hiyo (mambo yote yatakayotokea) mpaka siku ya Kiyama)) Imaam Ahmad, Abu Dawuud na At-Tirmidhy
Makadirio hayo yaliandikwa miaka khamsini kabla ya kuanza kuumba mbingu na ardhi
)) عن عبد الله بن عمرو بن العاص قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول كتب الله مقادير الخلائق قبل أن يخلق السموات والأرض بخمسين ألف سنة قال وعرشه على الماء)) مسلم .
((Kutoka kwa Abdullah Bin 'Umar bin Al-'Aas kasema, nimemsikia Mtume صلى الله عليه وسلم anasema Allaah سبحانه وتعالى ameandika makadirio ya viumbe kabla ya kuumba mbingu na ardhi miaka khamsini alfu, akasema na 'Arshi Yake ilikuwa katika maji)) Muslim
}}هُوَ الَّذِي خَلَق السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاء{{
{{ Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji }} Huud:7
Kwa hiyvo kutokana na hadithi hizo na qauli za Maulamaa wengi, kwamba kitu cha kwanza ilikuwa ni 'Arshi katika maji, kisha kalamu ambayo iliandika makadirio yote, kisha tena ndio mbingu na ardhi. Wallaahu A'alam.
Na hadithi ya Imaam Bukhari inathibitisha vile vile hayo:
((عن عمران بن حصي قال: قال أهل اليمن لرسول الله صلى الله عليه وسلم جئناك لنتفقه في الدين ولنسألك عن أول هذا الأمر فقال كان الله ولم يكن شيء قبله: وفي رواية معه وفي رواية غيره: وكان عرشه على الماء وكتب في الذكر كل شيء وخلق السموات والأرض : وفي لفظ :ثم خلق السموات والأرض ))البخاري
((Kutoka kwa 'Umar bin Haswiin ambaye kasema, walikuja wageni kutoka Yemen walimuuliza Mtume صلى الله عليه وسلم : tumekuja kijifunza dini na kukuuliza jambo la mwanzo, (yaani kabla ya kuumbwa kitu) akasema, Alikuwa Allaah, na hakukuwa na kitu kabla Yake, (Na Riwaya nyingine) na 'Arshi Yake ilikuwa katika maji, akaandika makadirio ya kila kitu, (Na kauli nyingine ) kisha akaumba mbingu na ardhi)) Al-Bukhaariy
Aya zifuatazo zinasema kuwa maumbo ya mwanzo yaliyoumbwa na Allaah سبحانه وتعالى ambayo yalitendeka kwa siku sita .
}}إِنَّ رَبَّكُمُ اللّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ أَلاَ لَهُ الْخَلْقُ وَالأَمْرُ تَبَارَكَ اللّهُ رَبُّ الْعَالَمِين{{
{{Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote}}
Al-A'araaf :54
}}اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْش{{
{{Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa siku sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi}} As-Sajda :4
Wataalamu wetu walizungumzia kuhusu siku sita hizi
Wengine wamesema ni siku za Allaah سبحانه وتعالى
}}وَإِنَّ يَوْمًا عِندَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ{{
{{Na hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni
Sheikh Al-Jazairiy amesema inaweza pia kuwa ni siku hizi zetu za kawaida kwani Allaah سبحانه وتعالى Ni Muweza wa kila kitu:
}}إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَنْ يَقُولَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ{{
{{Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa}}
Yasiin :82
Hadithi hii Sahihi imesimuliwa na Muslim inaelezea taratibu za maumbile katika wiki yalivyokuwa:
((عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ أَخَذَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِيَدِي فَقَالَ خَلَقَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ التُّرْبَةَ يَوْمَ السَّبْتِ وَخَلَقَ فِيهَا الْجِبَالَ يَوْمَ الأَحَدِ وَخَلَقَ الشَّجَرَ يَوْمَ الإِثْنَيْنِ وَخَلَقَ الْمَكْرُوهَ يَوْمَ الثُّلاثَاءِ وَخَلَقَ النُّورَ يَوْمَ الأََرْبِعَاءِ وَبَثَّ فِيهَا الدَّوَابَّ يَوْمَ الْخَمِيسِ وَخَلَقَ آدَمَ عَلَيْهِ السَّلاَم بَعْدَ الْعَصْرِ مِنْ يَوْمِ الْجُمُعَةِ فِي آخِرِ الْخَلْقِ فِي آخِرِ سَاعَةٍ مِنْ سَاعَاتِ الْجُمُعَةِ فِيمَا بَيْنَ الْعَصْرِ إِلَى اللَّيْلِ)) مسلم
((Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم alionyesha kwa mkono wake akasema, Allaah سبحانه وتعالى Ameumba udongo siku ya Jumamosi, Akaumba majabali siku ya Jumapili, Akaumba miti siku ya Jumatatu, Akaumba makirihisho (yaani mambo ya kukirihisha yote, na vidudu (Germs) na maradhi) siku ya Jumanne, Akaumba mwangaza siku ya Jumatano, Akaeneza wanyama siku ya Alkhamisi, Akaumuumba Adam عليه السلام baada ya Alasiri siku ya Ijumaa katika mwisho wa kuumba kwenye saa ya mwisho ya Ijumaa baina ya Alasiri na Usiku)) Muslim
Qatada alisema, Mayahudi walisema kwamba Allaah سبحانه وتعالى aliumba maumbile yote kwa siku sita kuanzia siku ya Jumapili kisha Akamalizia Ijumaa kwa hiyo alichoka akapumzika siku ya Jumamosi ndio maana wakaifanya Jumamosi kuwa ni siku
( At-Tabari 22:376)
}}وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالأََرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ{{
{{Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina
Uthibitisho mwengine wa kuwa Allaah سبحانه وتعالى hakuchoka kuumba chochote:
}}أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَمْ يَعْيَ بِخَلْقِهِنَّ بِقَادِرٍ عَلَى أَنْ يُحْيِيَ الْمَوْتَى بَلَى إِنَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ{{
{{Je! Hawaoni ya kwamba Mwenyezi Mungu, aliye ziumba mbingu na ardhi, na hakuchoka kwa kuziumba, kuwa ni Muweza wa kuwafufua wafu? Kwani? Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu}} Al-Ahqaaf:33
Wallaahu A'alam
Vimekusanywa kutoka:
1)Tafsiyr Ibn Kathiyr
2) At-Twabariy
3) Aysarut-tafaasiyr (Sh Abubakkar Al-Jazaairiy)
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
