05-Shaykh Al-Ghudayyaan: Msafiri Kuswali Rawaatib Katika Ramadhwaan

Msafiri Kuswali Rawaatib Katika Ramadhwaan

 

Shaykh Al-Ghudayyaan

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI: 

Je, msafiri ataswali swalah ya Rawaatib (Swalaah za Sunnah) katika mwezi wa Ramadhwaan, na vipi kuhusu thawabu kutokana na mwezi huu? 

 

JIBU:

Msafiri katika Ramadhwaan ataswali Dhuhr na Alasiri pamoja na afupishe (yaani dhuhr rakaa 2 na Alasiri 2). Na atasawli Maghrib rakaa 3  aichange na ‘Ishaa kwa kuswali rakaa 2;  wala asiswali Rawaatib (Swalaah za Sunnah). Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaposafiri, alikuwa anaswali (Sunnah ya) Witr na Rakaa mbili za asubuhi tu. Na ni maalumu kuwa msafiri na mgonjwa (kutokana na hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wanaandikiwa wote thawabu kwa yale ambayo walikuwa na ada kuyafanya kama wakaazi. Kwa msafiri, huandikia thawabu ya Swalaah yake kikamilifu, na huandikiwa thawabu ya kila Swalaah ambayo ameiswali kwa wakati wake. Endapo atajumuisha na kufupisha. Kwa mfano (alipokuwa kwake) alikuwa akiswali Swalaah ya Dhwuhaa n.k, huandikia thawabu kwa yale yote aliyokuwa akiyafanya kama mkaazi kwa sababu yuko safirni. Hali kadhalika kwa mgonjwa huandikiwa kwa yale alikuwa akiyafanya wakati alikuwa na afya yake.

 

 

Share