07-Shaykh Al-Luhaydaan: Muislamu Kufungua Mgawaha (Hoteli) Au Duka Mchana Wa Ramadhwaan

Muislamu Kufungua Mgawaha (Hoteli) Au Duka Mchana Wa Ramadhwaan

 

Shaykh Al-Luhaydaan

 

www.alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Ipi hukmu ya Muislamu kufungua Mgahawa (hoteli) mji wa makafiri mchana wa Ramadhwaan kwa ajili ya kuwauzia makafiri sehemu ambapo kunaishi Waislamu pia. Je, inajuzu?

 

JIBU:

 

 Ndio, hakuna matatizo kwa Muislamu kufungua mgahawa wake au duka ambalo wanauza chakula n.k, kwa kuwauzia wale ambao hawaingii katika hii hukmu (ya kufunga) kama Mayahudi, Manaswara, (Waislamu Wasafiri n.k), lakini asiwauzie chakula Waislamu ambao wamefunga. Asiwauzie Waislamu ambao anajua kabisa kwamba watakila mchana, ama akijua kuwa atakihifadhi chakula hicho mpaka wakati wa adhaana hakuna tatizo (kumuuzia). Hakuna ubaya kwake kuwauzia chakula au kinywaji hata Waislamu ambao hawakuwajibika na Swawm mchana wa Ramadhwaan. 

 

 

Share