08-Imaam Bin Baaz: Tofauti Ya Taraawiyh, Qiyaamul-Layl Na Tahajjud

Tofauti Ya Taraawiyh, Qiyaamul-Layl Na Tahajjud

 

Imaam Bin Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ipi tofauti kati ya Taaraawiyh, Qiyamul-Layl naTahajjud?

 

 

JIBU:

 

Swalah ya usiku huitwa Tahajjud na huitwa  Qiyamul-Layl kama Anavyosema. Allaah (Ta'aalaa):

 

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾

Na katika usiku, amka uswali nayo (tahajjud) ni ziada ya Sunnah kwako. Asaa Rabb wako Akakuinua cheo kinachosifika. [Al-Israa 17: 79]

 

Na Anasema (Subhaanahu):

 

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ﴿١﴾

Ee uliyejifunika. [Al-Muzzammil 73: 1-2]

 

 

 Na Anasema (Subhaanahu) katika Suwrah Adh-Dhaariyaat kuhusu waja wenye taqwa:

 

آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ﴿١٦﴾

Wakichukua yale Atakayowapa Rabb wao. Hakika wao walikuwa kabla ya hapo ni wahisani.

 

 

كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ﴿١٧﴾

Walikuwa kidogo tu katika usiku wakilala kwa raha.  [Adh-Dhaariyaat  51: 16-17]

 

 

Ama kuhusiana na Taraawiyh, ‘Ulamaa wanaiita Qiyamul-Layl katika ile sehemu ya kwanza ya usiku katika Ramadhwaan kwa ajili yake, kwa kuwa Swalaah hii haiswaliwi kwa muda mrefu tena.  Na inajuzu kuiita  Tahajjud au Qiyamul-Layl wala hakuna shaka katika hilo.

 

 

[Al-Mawqi' Ar-Rasmiy -  Imaam ‘Abdul-‘Aziyz Bin Baaz]

 

 

Share