04-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Imemjia Hedhi Dakika Chache Kabla Ya Magharibi Nini Hukmu Ya Swawm Yake?

Imemjia Hedhi Dakika Chache Kabla Ya Magharibi Nini Hukmu Ya Swawm Yake?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

Hukmu ya mwanamke aliyefunga amepata hedhi dakika  chache tu kabla ya kuzama jua (Magharibi).

 

 

JIBU: 

 

Ikiwa hedhi imeanza wakati mwanamke amefunga hata ikiwa ni dakika moja basi Swawm yake haifai na itambidi ailipe siku ile. Haruhusiwi kufunga wakati yuko kwenye hedhi, na akifunga basi Swawm yake haifai.

 

 

[Imaam Ibn 'Uthaymiyn - Majaalis Shahr Ramadhwaan, Ukurasa 39]

 

 

Share