06-Imaam Ibn Baaz: Imemjia Hedhi Dakika Tano Kabla Ya Magharibi Akidhi Swalaah Ya Magharibi?

Imemjia Hedhi Dakika Tano Kabla Ya Magharibi

 

Akidhi Swalaah Ya Magharibi Baada Ya Kutoharika?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

Nimefunga siku moja katika Ramadhwaan na haikubaki kitu siku hiyo isipokuwa dakika tano tu kufikia wakati wa kufuturu ikanijia hedhi ya mwezi. Je, ninawajibika kuswali Swalaah ya Magharibi kama kukidhi baada ya kutwaharika au la?

 

 

JIBU: 

 

Ikiwa hedhi imemjia kabla ya Magharibi kuingia basi haimuwajibikii kuswali Swalaah ya Magharibi wala Swalaah nyinginezo.

 

Na Swawm pia siku hiyo haitosihi, siku ambao imemjia hedhi kabla ya kuzama jua kwani swawm imebatilika na imemuwajibikia kulipa siku hiyo, ikiwa anajua kuwa imemjia hedhi kabla ya  Magharibi kuingia.

 

 

[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy - Imaam Ibn Baaz]

 

 

Share