13-Shaykh Swaalih Al-Luhaydaan: Mwenye Mimba Na Mnyonyeshaji Walipe Swawm Au Walishe Masikini?

Mwenye Mimba Na Mnyonyeshaji Walipe Swawm Au Walishe Masikini?

 

Shaykh Swaalih Al-Luhaydaan

www.alhidaaya.com

 

 
SWALI: 

Mwanamke anauliza pamoja na dada yake. Yeye ni mja mzito na dada yake ananyonyesha. Wanauliza kama wanaingia katika hukmu ya mgonjwa au inatosha kwao kulisha maskini kwa kila siku moja bila ya kulipa siku hizo? 

 

 

JIBU:

 

Mwenye mimba na mwenye kunyonyesha, wakikhofia madhara  kwenye afya zao, hukmu yao itakuwa kama ya mgonjwa itabidi wale na wasifunge.

Ama ikiwa atakuwa na khofu kwa ajili ya mtoto aliye tumboni au kijusu, basi ni juu yao kulipa siku hizo na walipe pia kafara. Na Kafara ni kulisha masikini mmoja kwa kila siku.

 

Na kuna ikhtilaaf katika masuala ya (kulisha) chakula. Kuna wanaosema akila sawa akiwa na khofu mwenyewe au na kwa mtoto wake watakula na hawatolisha masikini, ama kuhusiana na kulipa siku zile ni jambo la waajib.

 

(Hatomlisha masikini) ikiwa yeye binafsi hakuweza kufunga siku miongoni mwa siku (kwa sababu za ki Shariy’ah) hapo ndipo ataingia kwenye hukmu ya mgonjwa. 

 

 

Share