20-Shaykh Al-Fawzaan: Kupeana Pongezi Za ‘Iyd Kabla Ya Siku Ya ‘Iyd Kufika

Kupeana Pongezi Za ‘Iyd Kabla Ya Siku Ya ‘Iyd Kufika

 

Shaykh Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Aliulizwa Ash-Shaykh Al-‘Allaamah Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah):

“Kumeenea baina ya watu katika masiku haya, jumbe mbalimbali kupitia simu za mikononi zilizokusanya makatazo ya kupongezana siku ya ‘Iyd kwa siku moja au mbili kabla; na kwamba hivyo ni bid’ah, je, ni ipi rai yako ee mwenye fadhila?”

 

Akajibu (Hafidhwahu Allaah):

“Sielewi maneno haya. Haya yanayoenezwa. Sielewi kama yana asli yoyote.

 

Na pongezi inaruhusiwa, katika siku ya ‘Iyd au baada yake. Ama kabla ya siku ya ‘Iyd, sielewi kwamba imepatikana kufanywa hilo na As-Salaf (waja wema waliotangulia); kwamba wao walikuwa wakipongezana siku kabla ya ‘Iyd kufika.

 

Vipi mtu atapongeza jambo ambalo halijafanyika? Pongezi huwa ni katika siku ya ‘Iyd yenyewe au baada yake. Pamoja na kuwa (jambo hili la kupongezana) hakuna dalili (iliyopokelewa kutoka kwa Rasuli ‘Alayhis Swalaatu was Salaam) kuhusu hilo, lakini Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema ‘Mimi sianzi (kupongeza), lakini namjibu atakayenianza kunipongeza.’

Na’am.”

 

http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/thnih.mp3

 

Share