16-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Je, Inajuzu Kufunga Sitta Za Shawwaal Katika Mwezi Wa Dhul-Qa’dah Ikiwa Na Deni La Mwezi Mzima?

Je, Inajuzu Kufunga Sitta Za Shawwaal Katika Mwezi Wa Dhul-Qa’dah

Ikiwa Na Deni La Mwezi Mzima?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

"Ikiwa mfano mtu alikuwa ana deni la mwezi mzima wa Ramadhwaan kwa sababu ya kuwa safarini, au kuuguwa au kutokana na kuzaa, kisha akafunga kulipa deni mwezi wa Shawwaal na ukamalizika mwezi wote kulipa tu, basi anaweza kufunga Swiyyaam za Sitta katika mwezi wa Dhul-Qa’dah...  Ama ikiwa amefanya upuuzi katika kulipa deni kisha siku zikampita asiweze kufunga deni la Ramadhwaan hadi ikafika mwisho wa Shawwaal kisha akataka kufuatilia Sitta za Shawwaal basi hii haijuzu kwake."

 

 

[Liqaat Al-Baab Al-Maftuwh (117)]

 

 

 

Share