079-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Ya Jirani Na Mke Au Mume Muovu, Mwana Anayedhibiti, Rafiki Khaini

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Kuomba Kinga Ya Jirani Na Mke Au Mume Muovu, Mwana Anayedhibiti, Rafiki Haini.

 

  Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ إنِّي أّعُوذُ بِكَ مِنْ جَارِ السُّوءِ، وَمِنْ زَوْجٍ تُشَيِّبُنِي قَبْلَ المَشِيبِ، وَمِنْ وَلَدٍ يَكُونُ عَليَّ رَبّاً، وَمِنْ مَالٍ يَكُونُ عَلَيَّ عَذَابَاً، وَمِنْ خَلِيْلٍ مَاكِرٍ عَيْنُهُ تَرَانِي، وَقَلْبُهُ يَرْعَانِي؛ إِنْ رَأَى حَسَنَةً دَفَنَهَا، وَإِذَا رَأَى سَيِّئَةً أَذَاعَهَا 

 الطبراني في الدعاء، 3/ 1425، برقم 1339، وهناد في الزهد، برقم 1038، وقال الألباني في سلسلة الأحاديث الصحيحة، 7/ 377، برقم 3137 :  قلت: وهذا إسناد جيد، رجاله كلهم من رجال التهذيب

Allaahumma inniy a’uwdhu Bika min jaaris-suw-i, wa min zawjin tushayyibuniy qablal-mashiybi, wa min waladin yakuwnu ‘alayya rabban, wamin maalin yakuwnu ‘alayya ‘adhaaban, wamin khaliylin ‘aynuhuu taraaniy wa qalbuhu yar’aaniy, in raa hasanah dafanahaa, wa idhaa raa sayyiah adhaa’ahaa

 

Ee Allaah, najikinga Kwako kutokana na jirani muovu, na kutokana na mke au mume atakayenisababisha uzee kabla ya uzee, na kutokana mwana atakayekuwa ni bwana kwangu anayenidhibiti, na kutokana na mali itakayokuwa ni adhabu kwangu, na kutokana na rafiki mwandani khaini; ambaye macho yake yananitazama lakini huku moyo wake unaniangaza kwa hila kiasi kwamba anapoona zuri  hulificha, lakini  anapoliona baya hulitangaza.

 

 [Atw-Twabaraaniy katika Ad-Du’aa (3//1425) [1339] na Hunaad katika Az-Zuhd (1038) na Al-Albaaniy amesema katika As-Silsilat Asw-Swahiyhah (7/377) [3137]:  Nimesema hii ni Isnaad nzuri, watu wake wote ni katika watu wa kuaminika]

 

 

 

Share