072-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Jinn: قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا

 

 

Sababu Za Kuteremshwa

(Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Suwrah Al-Jinn

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

072-Al-Jinn

 

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾

1. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza; wakasema: ‘Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu.”

 

يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا﴿٢﴾

2. “Inaongoza kwenye uongofu, basi tukaiamini, na wala hatutomshirikisha Rabb   wetu na yeyote.”

 

 

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ انْطَلَقَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فِي طَائِفَةٍ مِنْ أَصْحَابِهِ عَامِدِينَ إِلَى سُوقِ عُكَاظٍ، وَقَدْ حِيلَ بَيْنَ الشَّيَاطِينِ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ، وَأُرْسِلَتْ عَلَيْهِمُ الشُّهُبُ، فَرَجَعَتِ الشَّيَاطِينُ إِلَى قَوْمِهِمْ‏.‏ فَقَالُوا: مَا لَكُمْ؟  فَقَالُوا: حِيلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ، وَأُرْسِلَتْ عَلَيْنَا الشُّهُبُ‏.‏ قَالُوا: مَا حَالَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ إِلاَّ شَىْءٌ حَدَثَ، فَاضْرِبُوا مَشَارِقَ الأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا، فَانْظُرُوا مَا هَذَا الَّذِي حَالَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ، فَانْصَرَفَ أُولَئِكَ الَّذِينَ تَوَجَّهُوا نَحْوَ تِهَامَةَ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ بِنَخْلَةَ، عَامِدِينَ إِلَى سُوقِ عُكَاظٍ وَهْوَ يُصَلِّي بِأَصْحَابِهِ صَلاَةَ الْفَجْرِ، فَلَمَّا سَمِعُوا الْقُرْآنَ اسْتَمَعُوا لَهُ فَقَالُوا : هَذَا وَاللَّهِ الَّذِي حَالَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ‏.‏ فَهُنَالِكَ حِينَ رَجَعُوا إِلَى قَوْمِهِمْ وَقَالُوا: يَا قَوْمَنَا ‏‏إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا‏ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَلَى نَبِيِّهِ صلى الله عليه وسلم ‏((‏قُلْ أُوحِيَ إِلَىَّ‏))‏ وَإِنَّمَا أُوحِيَ إِلَيْهِ قَوْلُ الْجِنِّ‏.‏

 

Musaddad ametuhadithia, amesema Abuu ‘Awaanah kutoka kwa Abuu Bishri kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضى الله عنهما) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na kundi la Maswahaba walitoka wakikusudia soko la ‘Ukaadhw, na wakati huo mashaytwaan walizuiwa khabari kutoka mbinguni na wakawa wanapigwa na vimondo, wakarudi kwao wakaambizana: Yamewatokea nini? Wakasema: tumezuiwa na khabari kutoka mbinguni, na tumepigwa na vimondo. Akasema: Hakuna kilichokuzuieni na khabari za mbinguni isipokuwa ni tukio lililotokea. Hivyo nendeni Mashariki ya ardhi na Magharibi yake muangalie ni jambo gani lililotokea. Hivyo wakaondoka na wakaenda Mashariki ya ardhi na Magharibi yake wakitafuta jambo lenyewe ambalo limewazuia na khabari za mbinguni. Wale walioelekea maeneo ya Tihaamah alipo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwenye mtende akikusudia soko la ‘Ukaadhw wakati huo akiswali pamoja na Maswahaba wake Swalaah ya Alfajiri. Pindi waliposikia Qur-aan ikisomwa walikaa kusikiliza wakasema: Hili ndilo lililotuzuia na khabari za mbinguni. Hapo ndipo waliporudi kwa watu wao wakasema: Enyi kaumu yetu! Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu. Inaongoza kwenye uongofu, basi tukaiamini, na wala hatutomshirikisha Rabb wetu na yeyote.” 

Allaah Akateremsha kwa Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم):

 قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ  

1. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Nimefunuliwa Wahy  

 

Kuwa imeshushwa wahyi kauli ya Jinni.

[Al-Bukhaariy Baab Al-Jahri Biqiraa-ati-Swalaatil-Fajri - Mlango wa kudhihirisha kisomo cha Swalaah ya Al-Fajr – Na Muslim usimulizi kama huo katika Baab Al-Jahri Bil-Qiraa-at Fiy Asw-Swubhi Wal-Qiraati ‘Alal-Jinn – Mlango wa kudhihirisha kisomo cha Swalaah ya Asubuhi na kisomo kwa Majini]

 

 

Baadhi Ya Aayah Katika Suwrah Al-Jinn:

 

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾

1. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza; wakasema: ‘Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu.”

 

يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا﴿٢﴾

2. “Inaongoza kwenye uongofu, basi tukaiamini, na wala hatutomshirikisha Rabb   wetu na yeyote.”

 

وَأَنَّهُ تَعَالَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا﴿٣﴾

3. “Na kwamba hakika umetukuka kabisa Ujalali wa Rabb wetu, Hakujifanyia mke wala mwana.”

 

وَأَنَّهُ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى اللَّـهِ شَطَطًا﴿٤﴾

4. “Na kwamba safihi miongoni mwetu alikuwa akisema juu ya Allaah uongo uliopinduka mipaka.”

 

وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن تَقُولَ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا﴿٥﴾

5. “Na kwamba sisi tulidhania wana Aadam na majini hawatosema uongo juu ya Allaah.”

 

وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا﴿٦﴾

6. “Na kwamba walikuwa wanaume miongoni mwa wana Aadam wanajikinga na wanaume miongoni mwa Majini, basi wakawazidishia madhambi, uvukaji mipaka ya kuasi na khofu.”

 

وَأَنَّهُمْ ظَنُّوا كَمَا ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَبْعَثَ اللَّـهُ أَحَدًا﴿٧﴾

7. “Na kwamba wao walidhania kama mlivyodhani kwamba Allaah Hatomfufua yeyote (au Hatomtuma Rasuli).”

 

وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا﴿٨﴾

8. “Na kwamba sisi tulitafuta kuzifikia mbingu, basi tukazikuta zimejaa walinzi wakali na vimondo.”

 

وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ ۖ فَمَن يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَّصَدًا﴿٩﴾

9. “Na kwamba sisi tulikuwa tukikaa huko vikao kwa ajili ya kusikiliza, basi atakayetega sikio kusikiliza sasa atakuta kimondo kinamvizia.”

 

وَأَنَّا لَا نَدْرِي أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِي الْأَرْضِ أَمْ أَرَادَ بِهِمْ رَبُّهُمْ رَشَدًا﴿١٠﴾

10. “Na kwamba sisi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa ardhini, au Rabb wao Anawatakia uongofu.”

 

وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا﴿١١﴾

11. “Na kwamba miongoni mwetu ni wema, na miongoni mwetu kinyume chake; tumekuwa makundi ya njia mbali mbali.”

 

وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن نُّعْجِزَ اللَّـهَ فِي الْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُ هَرَبًا﴿١٢﴾

12. “Na kwamba tulikuwa na yakini kwamba hatutoweza kumshinda Allaah ardhini, na wala hatutoweza kumkwepa kutoroka.”

 

وَأَنَّا لَمَّا سَمِعْنَا الْهُدَىٰ آمَنَّا بِهِ ۖ فَمَن يُؤْمِن بِرَبِّهِ فَلَا يَخَافُ بَخْسًا وَلَا رَهَقًا﴿١٣﴾

13. “Na kwamba sisi tuliposikia mwongozo (huu Qur-aan) tukaiamini; basi atakayemuamini Rabb wake hatoogopa kupunjwa mazuri yake na wala kuzidishiwa adhabu ya madhambi.”

 

 

Share