04-Ruqyah: Du’aa Za Kujiombea Au Kumuombea Mgonjwa

 

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Ruqyah: Du’aa Za  Kujiombea Au Kumuombea Mgonjwa

 

www.alhidaaya.com

 

 

Du’aa zifuatazo, anaweza aliye mgonjwa kujiombea mwenyewe au kumsomea mgonjwa mwengine.

 

 

Unapopata maumivu mwilini

Kwanza: Weka mkono wako juu ya sehemu inayouma kisha useme mara tatu:

 

بِسْمِ الله  أَعُوذُ بِاللَّهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ

BismiLLaah, A’uwdhu biLLaahi wa-Qudratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru

((Kwa jina la Allaah, Najikinga kwa Allaah na kwa uwezo Wake kutokana na shari ya ninachokisikia na ninachokiogopa)) [Hadiyth ya ‘Uthmaan bin Abiy Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu)  - Muslim (4/1728) [2202],  Ibn Maajah na wengineo kwa usimulizi tofauti kidogo]

 

Pili: Unaweka vidole vyako katika ardhi kugusa au chovya mchanga, kisha upangusie sehemu ya mwili yenye maumivu au maradhi na useme:

 بِسْمِ اللَّهِ، تُرْبَةُ أَرْضِنَا، بِرِيقَةِ بَعْضِنَا، يُشْفَى سَقِيمُنَا بِإِذْنِ رَبِّنَا

BismiLlaahi turbatu ardhwinaa, biriyqati ba’dhwinaa, yushfaa saqiymunaa biidhni Rabbinaa

 

((Kwa Jina la Allaah, mchanga ya ardhi yetu, kwa mate ya baadhi yetu, yanaponyesha mgonjwa wetu, kwa idhini ya Rabb wetu)). [Al-Bukhaariy, Muslim, Abuu Daawuud, Ibn Maajah, Ahmad]

 

Du’aa nyenginezo za kusoma:

 

 اللَّهُمَّ أَذْهِبْ الْبَاسَ، رَبَّ النَّاسِ، اشْفِ وَأَنْتَ الشَّافِي، لاَ شِفَاءَ إلاَّ شِفَاؤُكَ، شِفَاءًلاَ يُغَادِرُ سَقَمًا

Allaahumma Adh-hibil-ba-asa, Rabban-naasi, Ishfi wa-Antash-Shaafiy, laa-shifaa illa Shifaauka, shifaa-llaa yughaadiru saqamaa

((Ee Allah, Ondosha maumivu, Rabb wa watu, Ponyesha Nawe ni Mponyeshaji, hakuna shifaa ila shifaa yako, shifaa isiyobakisha maradhi)) [Al-Bukhaariy, Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad]

 

Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoingia kumzuru mgonjwa akimwambia:

لا بأْسَ طَهـورٌ إِنْ شـاءَ الله

Laa ba-asa twahuwrun In Shaa Allaah

((Hakuna neno, (ugonjwa) ni kusafishwa (na madhambi) Akipenda Allaah)) [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas  (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa)  - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (10/118) [3616]

 

Na kumuombea mgonjwa uliye naye au unapomtembelea du’aa ifuatayo mara saba.

 أَسْـأَلُ اللهَ العَـظيـم، رَبَّ العَـرْشِ العَـظيـم أَنْ يَشْفِـيَكَ

As-alu-LLaahal-‘Adhwiym, Rabbal-‘Arshil-‘Adhwiym, an Yashfiyak  

Namuomba Allaah Mtukufu Rabb wa ‘Arshi Tukufu Akuponyeshe.  [Hadiyth ya ‘Abdullaahi bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ’anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hapana mja yeyote Muislamu anayemtembelea mgonjwa ambaye wakati wake wa kufa bado haujafika na akamuombea mara saba, isipokuwa  Allaah Humponyesha mgonjwa huyo)). [At-Tirmidhiy [2083], Abuu Daawuwd [3106], Tazama pia Swahiyh At-Tirmidhiy (2/210), Swahiyh Al-Jaami’ (5/180) [5766]

 

 

 

 

Share