09-Ruqyah: Kuomba Kinga Kwa Allaah Dhidi Ya Adui, Dhulma, Na Ukandamizaji

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Kuomba Kinga Kwa Allaah Dhidi Ya Adui, Dhulma, Na Ukandamizaji

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Du’aa ifuatayo ni ya mwenye kuogopa dhulma ya anayetawala au ukandamizaji au dhidi ya yeyote unayekhofia dhulma zake. Unaisoma (hiyo du'aa) kisha unataja jina la mtu huyo.

 

أللَّهُمَّ رَبَّ السَّمواتِ السَّبْعِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيم، كُنْ لِي جاَراً مِنْ (فُلانِ بْنِ فُلاَنٍ) وَأَحْزَابِهِ مِنْ خَلاَئِقِكَ أَنْ يَفْرُطَ عَلَيَّ أحَدٌ مِنْهُمْ أَوْ يَطْغَى، عَزَّ جاَرُكَ وَجَلَّ ثَناَؤُكَ، وَلاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ

Allaahumma Rabbas-samaawatis-sab-’i wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwiym, kun liy jaaran min (fulaani bin fulaani – unamtaja jina lake) wa ahzaabihi min Khalaaiqika an yafrutwa ‘alayya ahadun minhum an yatw-ghaa. ‘Azza Jaaruka, wa Jalla Thanaauka, walaa ilaaha illaa Anta

 

Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba, na Rabb wa ‘Arshi Tukufu, kuwa Mlinzi wangu kutokana na (fulani bin fulani [taja mtu unayemhofu])  na vikosi vyake miongoni mwa viumbe Vyako, kwa kunisaliti mmoja miongoni  mwao, au kunifanyia uadui. Imeimarika madhubuti hifadhi Yako, na zimetukuka sifa Zako na hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe[Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) - Al-Bukhaariy fiy Al-Adab Al-Mufrad [707] na ameisahihisha Al-Albaaniy (  katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad [546].   

 

Du’aa nyingineyo ambayo pia unataja jina la mtu unayeogopa dhulma zake:

 

الله أكْبَر، الله أعَزُّ مِنْ خَلْقِهِ جَمِيْعاً، الله أعَزُّ مِمَّا أخَافُ وَأحْذَر، أعُوذُ بِاللهِ الَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ، الْمُمْسِكِ السَّمَوَا تِ السَّبْعِ أَنْ يَقَعْنَ عَلَى الأَرْضِ ِإلاَّ بِإِذْنِهِ، مِنْ شَرِّ عَبْدِكَ (فلان) وَجُنُوْدِهِ وَأَتْبَاعِهِ وَأَشْيَاعِهِ، مِنَ اْلجِنِّ والإِنْسِ، اَلَّلهُمَّ كُنْ لِيْ جَاراً مِنْ شَرِّهِمْ، جَلَّ ثَنَاؤُكَ وَعَزَّ جَارُكَ، وَتَبَارَكَ اسْمُكَ، وَلاَ إلَهَ غَيْرُكَ

Allaahu Akbar, Allaahu A’azzu min Khalqihi jamiy’aa. Allaahu A’azzu mimmaa akhaafu wa ahdharu. A’uwdhu biLLaahi Alladhiy laa ilaaha illaa Huwa. Al-Mumsikis-samawaatis-sab-’i an yaqa’-na ‘alal-ardhwi illaa biidhnihi, min sharri ‘abdika (fulani - mtaje mtu unayemkhofu) wa junuwdihi, wa atbaa’ihi, wa ash-yaa’ihii minal jinni wal insi. Allaahumma kun-liy jaaran min sharrihim, Jalla Thanaauka, wa ‘Azza Jaaruka, wa Tabaarakas-Smuka walaa ilaaha Ghayruka [mara 3].

 

Allaah ni Mkubwa, Allaah, ni Mwenye ni Mwenye nguvu Mshindi kuliko viumbe Vyake vyote. Allaah ni Mwenye nguvu Mshindi kuliko kila nikiogopacho na kujihadhari. Najikinga kwa Allaah Ambaye hapana muabudiwa wa haki ila Yeye tu, Ambaye Ameshikilia mbingu saba ili zisiangukie ardhi ila kwa idhini Yake, kutokana na shari ya mja (fulani - mtaje mtu unayemkhofu) na majeshi yake, na wanaomfuata, na wafuasi wake miongoni mwa majini na watu. Ee Allaah, kuwa Mlinzi wangu kutokana na shari yao. Zimetukuka Sifa Zako na Umetukuka ulinzi Wako na Limebarikika Jina Lako, na hapana muabudiwa wa haki ghairi Yako. [Du’aa ya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) Al-Bukhaariy fiy Adabil-Mufrad [708] na ameisahihisha Al-Albaaniy  katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad [546].]

 

 

Du’aa nyinginezo:

 

 اَللَّهُمَّ احْفَظْنِي بِالإِسْلاَمِ قَائِمًا  وَاحْفَظْنِي بِالإِسْلاَمِ قَاعِداً  وَاحْفَظْنِي بِالإِسْلاَمِ رَاقِداً  وَلاَ تُشْمِتْ بِي عَدُوًا وَلاَ حَاسِداً. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ كُلِّ خَيْرٍ خَزَائِنُهُ بِيَدِكَ  وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ كُلِّ شَرٍّ خَزَائِنُهُ بِيَدِك   

Allaahummah-fadhwniy bil Islaami qaaimaa, wahfadhwniy bil Islaami qaaidaa, wahfadhwniy bil Islaami raaqidaa, walaa tushmit biy ‘aduwwan walaa haasidaa. Allaahumma inniy as-aluka min kulli khayrin khazaainuhu Biyadika, wa a’uwdhu Bika min kulli sharrin khazaainuhu Biyadika

 

Ee Allaah, nihifadhi katika Uislamu nikiwa nimesimama, na nihifadhi katika Usilamu nikiwa nimekaa, na nihifadhi katika Uislamu nikiwa nimelala, wala Usinijaalie kuwa bezo la adui wala hasidi. Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kila khayr ambazo hazina zake zimo Mikononi Mwako, na najikinga Kwako shari zote ambazo hazina zake zimo Mikononi Mwako. [Al-Haakim, Taz., Swahiyh Al-Jaami’ (2/398) na Silsilat Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (4/54 – 1540)]

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ غَلَبَةِ الدَّيْنِ وَغَلَبَةِ الْعَدُوِّ وَشَمَاتَةِ الأَعْدَاءِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min ghalabatid-dayni, wa ghalabatil-‘aduwwi wa shamaatatil-a’-daai

 

Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako kushindwa deni, na kushindwa na adui, na bezo la maadui.  [An-Nasaaiy, Ahmad -  Swahiyh An-Nasaaiy (3/1113)]

 

أللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ جَهْدِ الْبَلاَءِ وَدَرَكِ الشَّقَاءِ وَسُوءِ الْقَضَاءِ وَشَمَاتَةِ الأَعْدَاءِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min jahdil-balaai wa darakish-shaqaai wa suw-il-qadhwaai, wa shamaatatil-a’daai

 

Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako shida ya balaa [mitihani n.k.] na kukumbwa na uovu na majaaliwa mabaya na bezo la maadui. [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْفَقْرِ وَالْقِلَّةِ وَالذِّلَّةِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أَظْلِمَ أَوْ أُظْلَمَ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-faqri wal-qillati, wadh-dhillati, wa a’uwdhu bika min an adhwlima aw udhwlama

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako ufakiri na uchache na udhalilifu na najikinga Kwako kudhulumu au kudhulumiwa. [Abuu Daawuwd, Ahmad – Swahiyh Abiy Daawuwd (1544)]

 

اللَّهُمَّ مَتِّعْنِي بِسَمْعِي وَبَصَرِي  وَاجْعَلْهُمَا الْوَارِثَ مِنِّي وَانْصُرْنِي عَلَى مَنْ يَظْلِمُنِي وَخُذْ مِنْهُ بِثَأْرِي

Allaahumma matti’-niy bisam-’iy, wa baswariy, waj-’al-humal-waaritha minniy, wanswurniy ‘alaa man yadhwlimuniy, wa khudh minhu bitha-ariy

 

Ee Allaah, ninufaishe kwa masikio yangu, na macho yangu, na vijaalie [viwili hivyo] viwe hivyo kwa warithi wangu na ninusuru dhidi ya anayenidhulumu, na nilipizie dhidi yake.[At-Tirmidhiy Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/188)]

 

حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

Hasbuna-Allaahu wa Ni’-mal-Wakiyl

 

Allaah Anatutosheleza, Mzuri Alioje Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.

[Al-Bukhaariy  kutoka kwa Ibn ‘Abbaas: “Ameisema Ibraahiym  ('Alayhis-Salaam) alipotupwa Motoni na ameisema Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) waliposema (Suwrat A’Imraan 3: 173) ((“Hasbuna-Allaah! Allaah Anatutosheleza, Mzuri Alioje Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.”)) 

 

اللَّهُمَّ لَكَ أَسْلَمْتُ وَبِكَ آمَنْتُ وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْكَ أَنَبْتُ وَبِكَ خَاصَمْتُ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِعِزَّتِكَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ أَنْ تُضِلَّنِي أَنْتَ الْحَيُّ الَّذِي لاَ يَمُوتُ وَالْجِنُّ وَالإِنْسُ يَمُوتُونَ

 

Allaahumma laka aslamtu, wa bika aamantu, wa ‘alayka tawakkaltu, wa ilayka anabtu, wa bika khaaswamtu. Allaahumma inniy a’uwdhu bika bi’izzatika laa ilaaha illa Anta an-tudhwillaniy Antal-Hayyu Alladhiy  laa Yamuwtu wal-jinnu wal-insu yamuwtuwna.

 

Ee Allaah, Kwako najisalimisha na Kwako naamini na Kwako natawakali na Kwako narejea kutubu na Kwako nagombana [dhidi ya adui]. Ee Allaah, hakika mimi najikinga kwa Utukufu Wako, hapana muabudiwa wa haki ila Wewe Usije kunipotoa Wewe Uliye Hai daima Ambaye Hafi ilhali majini na watu wanakufa.

[Muslim, Ahmad]

 

رَبِّ أَعِنِّي وَلاَ تُعِنْ عَلَيَّ، وَانْصُرْنِي وَلاَ تَنْصُرْ عَلَيَّ، وَامْكُرْ لِي وَلاَ تَمْكُرْ عَلَيَّ، وَاهْدِنِي وَيَسِّرْ الْهُدَى إِلَيَّ ، وَانْصُرْنِي عَلَى مَنْ بَغَى عَلَيَّ،  رَبِّ اجْعَلْنِي لَكَ شَكَّارًا، لَكَ ذَكَّارًا، لَكَ رَهَّابًا، لَكَ مُطِيعًا، إِلَيْكَ مُخْبِتًا أَوَّاهًا مُنِيبًا، رَبِّ تَقَبَّلْ تَوْبَتِي، وَاغْسِلْ حَوْبَتِي،  وَأَجِبْ دَعْوَتِي، وَثَبِّتْ حُجَّتِي، وَاهْدِ قَلْبِي، وَسَدِّدْ لِسَانِي، وَاسْلُلْ سَخِيمَةَ قَلْبِي  

 

Rabbi a’inniy walaa tu’in ‘alayya, wanswurniy walaa tanswur ‘alayya, wamkur-liy walaa tamkur ‘alayya, wahdiniy wa yassiril-hudaa ilayya, wanswurniy ‘alaa man baghaa ‘alayya. Rabbij-’alniy Laka shakkaaraa, Laka dhakkaaraa, Laka Rahhaaba, Laka mutwi’y-aa, ilayka mukhbitan awwaaham-muniybaa. Rabbi taqabbal tawbatiy, waghsil hawbatiy, wa ajib da’-watiy wahdi qalbiy, wa saddid lisaaniy, wa thabbit hujjatiy, waslul sakhiymata qalbiy.

 

Ee Rabb wangu nisaidie na Usisaidie dhidi yangu, na ninusuru wala Usinusuru dhidi yangu, na nipangie na Usipange dhidi yangu, na niongoze na usahilishe hidaaya kunijia na ninusuru dhidi ya atakayenifanyia uovu. Rabb wangu nijaalie niwe mwenye kukushukuru, mwenye kukudhukuru, mwenye kukuogopa, mwenye kukutii, mwenye kukukhofu, mwenye kunyenyekea na kurudia kuomba tawbah. Rabb wangu pokea tawbah yangu, na osha madhambi yangu, na Itikia du’aa zangu, na thibitisha hoja zangu, na Uhidi moyo wangu, na Nyoosha ulimi wangu [useme kweli], na futa uovu wa moyo wangu. [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah – Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/178) na Ahmad (1/127)]

 

 

Share