Shaykh Fawzaan: Amemaliza Hedhi Akiwa Safarini Katika Ndege Afanye Wudhuu Ili Aswali?

 

Amemaliza Hedhi Akiwa Safarini Katika Ndege Afanye Wudhuu Ili Aswali?

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Mwanamke amemlaiza hedhi yake akiwa safarini katika ndege, (basi akitaka kuswali) je inamtosheleza kufanya wudhuu kwa ajili ya kuswali?

 

 

JIBU:

 

Hapana! Angojee mpaka ndege iteremke (afike kwake) ambako ataweza kufanya ghuslu kisha ndio aswali. Ikiwa anakhofia kuwa wakati wa Swalaah utampita akiwa katika ndege kwa sababu ni safari ndefu, basi anaweza kufanya tayammum ikiwa atapata vumbi la kutumia mikononi mwake kisha aswali. Ikiwa atapata vumbi basi afanye tayammum, lakini kama hakupata vumbi lolote na safari ni ndefu basi aswali bila ya kuoga kwani Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema:

 

 Basi mcheni Allaah muwezavyo. [At-Taghaabun : 16]

 

[Sharh ‘Umdatil-Fiqh Shariytw (7, Swali Namba 17)]

Share