Imaam Ibn Al-Qayyim: Vile Unavyomfanyia Mwana Aadam Mwenzako Ndivyo Allah Atakufanyia

Vile Unavyomfanyia Mwana Aadam Mwenzako Ndivyo Allah Atakufanyia

 

Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn Qayyim Al-Jawziyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Atakayewafanyia upole waja wa Allaah, basi Allaah Atamfanyia upole.

Atakayewarehemu, basi naye Allaah Atamrehemu.

Na atakayewafanyia ihsaan, basi naye Allaah Atamfanyia ihsaan.

Na atakayewafanyia ukarimu, basi naye Allaah Atamfanyia ukarimu.

Na Atakayewanufaisha, basi naye Allaah Atamnufaisha.

Na atakayewasitiri, basi naye Allaah Atamsitiri,

Na Atakayewanyima khayr, basi naye Allaah Atamnyima khayr.

Na atakayewafanyia viumbe Wa Allaah (mema) kwa sifa ambazo Allaah Huwafanyia (waja Wake) basi (Allaah) Atamsaidia duniani na Aakhirah.  Kwani Allaah (Ta’aalaa) Humfanyia mja vile vile kama mtu anavyowafanyia viumbe Wa Allaah.”

 

 

[Al-Waabil Asw-Swayyib, uk. 35)]

 

 

Share