Imaam Ibrahiym Bin Ad-ham: Mambo Kumi Kwanini Du’aa Zetu Hazitakabaliwi

Mambo Kumi Kwanini Du’aa Zetu Hazitakbaliwi

 

Imaam Ibraahiym Bin Ad-ham (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibraahiym bin Ad-ham alipitia sokoni wakajumuika watu kumuliza: “Ee Abaa Is-haaq! Kwa nini du’aa zetu hazitakabaliwi?”

 

Alijibu: “Kwa sababu nyoyo zenu zimekufa kwa mambo kumi:

 

1-Mnamjua Allaah lakini hamtimizi haki Zake.

 

2- Mnajidai kumpenda Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) lakini mkaacha Sunnah zake.

 

3-Mnaisoma Qur-aan lakini hamtekelezi yaliyomo.

 

4- Mnakula katika neema za Allaah, lakini hamshukuru.

 

5-Mnasema shaytwaan ni adui yenu lakini mnaandamana naye.

 

6-Mnadai kuwa Jannah ni haki, (mnaitamani), lakini hamuifanyii kazi.

 

7-Mnadai mnaujua Moto lakini hamjiepushi nao.

 

8-Mnasema mauti ni haki yatawafika tu, lakini hamtayarishi nafsi zenu kwayo.

 

9-Mnashughulika na usingizi na aibu za watu mnaacha zenu.

 

10-Mnazika maiti zenu lakini hamzingatii kwayo.”

 

[Jaami’ Bayaan Al-‘Ilm wa Fadhwlih (2/12)]

 

 

 

Share