017-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Anfaal Aayah 017: فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ قَتَلَهُمْ ۚ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ رَمَىٰ

 

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

Al-Anfaal:  17

 

 

 

17- Hamkuwaua nyinyi, lakini Allaah Ndiye Aliyewaua. Na wala hukurusha...

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

  

فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ قَتَلَهُمْ ۚ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ رَمَىٰ ۚ وَلِيُبْلِيَ الْمُؤْمِنِينَ مِنْهُ بَلَاءً حَسَنًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١٧﴾

 

Hamkuwaua nyinyi, lakini Allaah Ndiye Aliyewaua. Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم  mchanga) pale uliporusha lakini Allaah Ndiye Aliyerusha, na ili Awajaribu Waumini jaribio zuri kutoka Kwake. Hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote. [Al-Anfaal: 17]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

  وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ رَمَىٰ ۚ  

Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم  mchanga) pale uliporusha lakini Allaah Ndiye Aliyerusha.

 

Amehadithia Hakiym bin Hizaam kwamba Imeteremshwa siku ya Badr pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoamrishwa, akateka changarawe za mawe mkononi, akatukabili nazo na kuturushia akisema: “Nyuso zinyauke!” Tukashindwa. Allaah (عز وجل) Akateremsha:

وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ رَمَىٰ ۚ  

Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم  mchanga) pale uliporusha lakini Allaah Ndiye Aliyerusha.   [Atw-Twabaraaniy]

 

 

 

Share