05-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kuingia Masjidul-Haraam Katika Mlango Mahsusi Na Du'aa Anapoona Ka'bah

 

 

Kuingia Masjidul-Haraam Katika Mlango Mahsusi Na Du'aa Anapoona Ka'bah

 

 Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

   

SWALI:

 

Makosa gani yanatendwa na Mahujaji wanapoingia Al-Masjidul-Haraam?

 

 

JIBU:

 

Miongoni mwa makosa yanayotendwa na Mahujaji wanapoingia Masjidul-Haraam ni yafuatayo:

 

Kwanza:

 

Baadhi ya watu wanaofanya Hajj au 'Umrah wanadhania  kuwa ni muhimu kuingia Masjidul-Haraam katika mlango mahsusi. Mfano wengine wanadhani kwamba kwa ajili ya 'Umrah shariy’ah inampasa mtu aingie katika Baab Al-Umrah  (mlango wa 'Umrah).  Wengine wanadhani kuwa ni muhimu kuingilia katika Baabus-Salaam (Mlango wa Amani) na kwamba kuingilia milango mingine ni dhambi au jambo lisilopendeza. Hakuna dalili yoyote inayotaja hivi, kwa hiyo anaweza mtu kuingilia mlango wowote uliokuwa karibu naye. Kinachompasa ni kufuata Sunnah kwa kuingia Msikitini kwa kutanguliza mguu wa kulia na kusema:

 

 

أَعُوذُ بِاللَّهِ الْعَظِيمِ, وَبِوَجْهِهِ الْكَرِيمِ, وَسُلْطَانِهِ الْقَدِيمِ, مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ. بِسْـمِ الله، وَالصَّلاةُ وَالسَّلامُ عَلى رَسولِ الله، اللّهُـمَّ افْتَـحْ لي أَبْوابَ رَحْمَتـِك

Najikinga na Allaah Aliye Mtukufu, na kwa Wajihi Wake Karimu, na kwa utawala Wake wa kale, kutokana na shaytwaan aliyeepushwa na Rehma za Allaah

Kwa jina la Allaa na Swalaah na Salaam zimfikie  Rasuli wa Allaah. Ee Allaah nifungulie milango ya Rehma Yako

 

Pili:

 

Baadhi ya watu wanazusha du'aa wanapoingia Masjidul-Haraam na wakati wa kuliona Ka'bah. Du'aa hizo ni za bid’ah kwa sababu hazikutajwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo ikiwa vitendo vyote vya ‘ibaadah ikiwa ni kauli au matendo havikupatikana dalili kutoka katika Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake huwa ni vya bid’ah na kuvitenda ni kutenda dhambi ambayo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya sana.

 

[Al-Bid’ah wal-Muhdathaat wa maa laa aswla lahu – Uk. 384, Fiqh al-'Ibaadaat – Uk. 344]

 

 

Share