01-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kumfanyia Hajj Mama Aliyekuwa Haswali Kabisa

 

Kumfanyia Hajj Mama Aliyekuwa Haswali Kabisa

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Je, inafaa mtoto wa kike kumfanyia Hajj na kumtolea sadaqah mama yake aliyefariki ambaye hakuwa akiswali katika uhai wake? Nini hukmu ya jambo hili ikiwa mtoto anataka kutimiza wajibu wake (wa kufawanyia wema wazazi) kama alivyopata mafunzo katika Dini yetu ya Kiislam? 

 

JIBU:

 

Yeyote anayeacha Swalaah makusudi kwa sababu hadhani kuwa ni fardhi kwake, atakuwa amekufuru kutokana na rai waliyokubaliana ‘Ulamaa.  Na yeyote anayeacha kuswali kwa sababu ya uvivu au kudharau, basi naye pia atakuwa amekufuru kutokana na rai za ‘Ulamaa wengi.   Hii ni kwa sababu Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

  ((إن العهد الذي بيننا و بينهم الصلاة فمن تركها فقد كفر )) أخرجه أصحاب السنن

((Mafungamano baina yetu na wao (Makafiri) ni Swalaah, atakayeiacha amekufuru)) [Abu Dawwuwd, At-Tirmidhy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

 

Juu ya hivyo, dalili nyingine kutoka katika Qur-aan na Sunnah zimethibiti hukmu hiyo.

 

Kwa hiyo, haipasi kumfanyia Hajj au kumtolea sadaqah mtu mwingine aliyekufa ambaye hakuwa akiswali, kama ilivyokuwa haifai kumfanyia Hajj au kutoa sadaqah kwa ajili ya Kafiri.

 

 

Wa-BiLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiy Muhammad wa Aswhaabihi wasallam.

 

[Fataawa Al-Lajnatud-Daaimah lil-buhuwthil-'Ilmiyyah wal-Iftaa Mjalada 11, Uk. 113, Swali Namba 2 ya Fatwa Namba 6178 - Imejumuishwa: 

 

Kiongozi Mkuu: Shaykh 'Abdul 'Aziyz ibn 'Abdillaah  ibn Baaz

 

Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy

 

Mjumbe: Shaykh 'Abdullaah Ibn Ghudayyaan

 

Mjumbe: Shaykh 'Abdullaah ibn Qu'uwd]

 

 

Share