09-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Hakukata Au Kunyoa Nywele Baada Ya Kumaliza Sa’y

 

Hakukata Au Kunyoa Nywele Baada Ya Kumaliza Sa’y

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

   

 

 

SWALI:

 

Aliyemaliza Hajj ya Tamattu'u alifanya Sa’y kisha akabadilisha nguo zake lakini hakukata au kunyoa nywele. Kisha baada ya Hajj aliuliza akaambiwa kwamba ni makosa. Nini inampasa afanye sasa kwa vile muda wa Hajj umekwishapita?

 

 

JIBU:

 

Atahesabika kuwa ameacha kitendo cha waajib katika vitendo vya fardhi vya 'Umrah, nacho ni kukata au kunyoa nywele. Kutokana na rai za ‘Ulamaa, inampasa atoe kafara nayo ni kuchinja na kugawa nyama kwa masikini na wahitaji wa Makkah na Hijja yake haitoharibika.

 

 

[Fataawa al-Hajj wal-'Umrah waz-Ziyaarah – Uk. 93]

 

 

Share