Vibiskuti Vya Matunda Makavu Na Cornflakes

Vibiskuti Vya Matunda Makavu Na Cornflake

VIPIMO

 

Unga -  4 Vikombe

Sukari -  1 Kikombe

Baking powder 1 kijiko cha chai mfuto

 Siagi  -  454 gms

 Mayai -   2

 Matunda makavu (tende, zabibu, lozi) - 1 Kikombe

 Vanilla - 2 Vijiko vya chai

 Cornflakes  -  ½ kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya sukari na siagi katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy)
  2. Tia yai moja moja huku unachanganya mpaka iwe laini kama sufi. (fluffy)
  3. Tia unga, baking powder, matunda makavu, changanya na mwiko.
  4. Chota mchanganyiko  wa biskuti kwa mkono kama (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara na uchovye katika cornflakes iliyopondwa   kwa mkono (crushed)
  5. Zipange katika treya ya kupikia na zipike (bake) katika  moto wa 375°F kwa muda wa kiasi dakika 15 huku unazitazama tazama.
KIDOKEZO
Unaweza kufanya nusu yake kwani zinatoka nyingi kipimo hicho.
 

 

 

 

 

 

 

 

Share