10-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Iqrari (Kukiri Kosa)

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

 

بَابُ اَلْإِقْرَارِ

10-Mlango Wa Iqrari[1] (Kukiri Kosa)

 

 

 

 

 

750.

عَنْ أَبِي ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ لِي رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {قُلِ اَلْحَقَّ، وَلَوْ كَانَ مُرًّا} صَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ فِي حَدِيثٍ طَوِيلٍ 

Kutoka kwa Abuu Dharr[2] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ameniambia: “Sema haki japo ni chungu.” [Kaisahihisha Ibn Hibbaan kutoka Hadiyth ndefu]

 

 


[1] Iqraar ni kuthibitisha kitu fulani, kulingana na Istwilaah ya kishariy’ah ni mtu kukubali aliyoyafanya. Ni kinyume na kukana au kukataa.

 

[2] Jina lake ni Jundub bin Junaadah, ni Swahaba alisilimu kitambo, imepokewa kuwa yeye alisema: “Mimi ni mtu wa tano katika Uislam.” Hupigiwa mfano katika ukweli, naye ndiye wa kwanza aliyemuamkia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) maakizi ya Kiislamu. Alifariki mwaka wa 32 Hijriyyah. Katika vitabu vya Hadiyth, ana Hadiyth 281.

 

 

Share