15-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Kumwagilia Musaaqaah Na Kukodisha

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

 

بَابُ اَلْمُسَاقَاةِ وَالْإِجَارَةِ

15-Mlango Wa Kumwagilia Musaaqaah[1] Na Kukodisha[2]

 

 

 

 

 

767.

عَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  عَامَلَ أَهْلَ خَيْبَرَ بِشَطْرِ مَا يَخْرُجُ مِنْهَا مِنْ ثَمَرٍ، أَوْ زَرْعٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.

وَفِي رِوَايَةٍ لَهُمَا: فَسَأَلُوا أَنْ يُقِرَّهُمْ بِهَا عَلَى أَنْ يَكْفُوا عَمَلَهَا وَلَهُمْ نِصْفُ اَلثَّمَرِ، فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ نُقِرُّكُمْ بِهَا عَلَى ذَلِكَ مَا شِئْنَا "، فَقَرُّوا بِهَا، حَتَّى أَجْلَاهُمْ عُمَرُ

وَلِمُسْلِمٍ:{أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ دَفَعَ إِلَى يَهُودِ خَيْبَرَ نَخْلَ خَيْبَرَ وَأَرْضَهَا عَلَى أَنْ يَعْتَمِلُوهَا مِنْ أَمْوَالِهِمْ، وَلَهُ شَطْرُ ثَمَرِهَا}   

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliamiliana na watu wa Khaybar (Mayahudi) kwa makubaliano kuwa atapewa nusu ya kitakachotoka humo kutokana na matunda au mazao.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Katika Riwaayah yao nyingine: “… (Mayahudi) Wakamuomba Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) awaache waishi (Khaybar) kwa sharti walime mali na yao iwe nusu ya tende. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Tumewaruhusu muishi kwa sharti hiyo mpaka tutakapotaka.” Akawaruhusu kuishi humo mpaka ‘’Umar alipowafukuza’

Katika Riwaayah ya Muslim: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwapa Mayahudi wa Khaybar mitende ya Khaybar na ardhi ya huko kwa sharti walime kwa mali yao nao wapate nusu ya matunda yake.”[3]

 

 

 

768.

وَعَنْ حَنْظَلَةَ بْنِ قَيْسٍ قَالَ:{سَأَلْتُ رَافِعَ بْنَ خَدِيجٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ كِرَاءِ اَلْأَرْضِ بِالذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ ؟ فَقَالَ: لَا بَأْسَ بِهِ، إِنَّمَا كَانَ اَلنَّاسُ يُؤَاجِرُونَ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  عَلَى الْمَاذِيَانَاتِ، وَأَقْبَالِ اَلْجَدَاوِلِ، وَأَشْيَاءَ مِنْ اَلزَّرْعِ، فَيَهْلِكُ هَذَا وَيَسْلَمُ هَذَا، وَيَسْلَمُ هَذَا وَيَهْلِكُ هَذَا، وَلَمْ يَكُنْ لِلنَّاسِ كِرَاءٌ إِلَّا هَذَا، فَلِذَلِكَ زَجَرَ عَنْهُ، فَأَمَّا شَيْءٌ مَعْلُومٌ مَضْمُونٌ فَلَا بَأْسَ بِهِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ  .

وَفِيهِ بَيَانٌ لِمَا أُجْمِلَ فِي اَلْمُتَّفَقَ عَلَيْهِ مِنْ إِطْلَاقِ اَلنَّهْيِ عَنْ كِرَاءِ اَلْأَرْضِ

Kutoka kwa Handhwalah bin Qays[4] amesema: “Nilimuuliza Raafi’ bin Khadiyj (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) juu ya kuikodisha ardhi kwa dhahabu na fedha. Akasema: “Hapana ubaya. Kwani watu walikuwa wakiajiriana wakati wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) sehemu zilizopo juu ya mito mikubwa na katika vianzio vya mito midogo na kwa sehemu ya mazao. Basi sehemu moja inaangamia,[5] na sehemu nyingine ikisalimika, na sehemu hii ikisalimika nyingine inaangamia. Watu walikuwa hawana upangaji isipokuwa huu. Kwa ajili hiyo kakataza. Ama kikikodishwa kwa kitu chenye kujulikana na chenye dhamana basi hakina ubaya.” [Imetolewa na Muslim]

Haya yanathibitisha yaliyokumuishwa katika Al-Bukhaariy na Muslim katika uharamu wa kukodisha ardhi.

 

 

 

769.

وَعَنْ ثَابِتِ بْنِ اَلضَّحَّاكِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ نَهَى عَنْ اَلْمُزَارَعَةِ  وَأَمَرَ بِالْمُؤَاجَرَةِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ أَيْضًا 

Kutoka kwa Thaabit bin Adhw-Dwahhaak[6] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza Muzaara’ah[7] na akaamrisha kuajiriana.”[8] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

770.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّهُ قَالَ: {اِحْتَجَمَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  وَأَعْطَى اَلَّذِي حَجَمَهُ أَجْرَهُ} وَلَوْ كَانَ حَرَاماً لَمْ يُعْطِهِ. رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliumika na akampa muumikaji ujira wake.” Lau ingalikuwa haraam basi asingalimpa. [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

771.

وَعَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {كَسْبُ اَلْحَجَّامِ خَبِيثٌ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Raafi’ bin Khadiyj (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Chumo la muumikaji ni chafu.”[9] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

772.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {قَالَ اَللَّهُ (عَزَّ وَجَلَّ) ثَلَاثَةٌ أَنَا خَصْمُهُمْ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ: رَجُلٌ أَعْطَى بِي ثُمَّ غَدَرَ، وَرَجُلٌ بَاعَ حُرًّا ، فَأَكَلَ ثَمَنَهُ، وَرَجُلٌ اِسْتَأْجَرَ أَجِيرًا ، فَاسْتَوْفَى مِنْهُ، وَلَمْ يُعْطِهِ أَجْرَهُ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah (عزّ وجلّ)      amesema: Watu watatu Mimi ni Mtesi wao siku ya Qiyaamah: mtu ametoa kwa jina Langu kisha akahini, mtu anamuuza muungwana na akala thamani yake, na mtu amemuajiri muajiriwa naye akamkamilishia kazi yake wala hakumpa ujira wake.”[10] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

773.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {إِنَّ أَحَقَّ مَا أَخَذْتُمْ عَلَيْهِ حَقًّا كِتَابُ اَللَّهِ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika cha haki zaidi mliochukua malipo juu yake ni Kitabu cha Allaah.”[11] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

774.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {أَعْطُوا اَلْأَجِيرَ أَجْرَهُ قَبْلَ أَنْ يَجِفَّ عَرَقُهُ} رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَهْ 

وفي الباب: عن أبي هريرة رضي الله عنه عند أبي يعلى والبيهقي. وجابر عند الطبراني، وكلها ضعاف

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mumpeni muajiriwa malipo yake kabla jasho lake kukauka.”[12] [Imetolewa na Ibn Maajah]

 

Katika mlangu huu kuna Hadiyth iliyopokewa na Abuu Hurayrah iliyo kwa Abuu Ya’laa na Bayhaqiyy na iliyopokewa kutoka kwa Jaabir iliyo kwa Atw-Twabaraaniy, Riwaayah zote ni dhaifu.

 

 

 

775.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: {مَنِ اِسْتَأْجَرَ أَجِيراً، فَلْيُسَلِّمْ لَهُ أُجْرَتَهُ} رَوَاهُ عَبْدُ اَلرَّزَّاقِ وَفِيهِ اِنْقِطَاعٌ، وَوَصَلَهُ اَلْبَيْهَقِيُّ مِنْ طَرِيقِ أَبِي حَنِيفَةَ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuajiri muajiriwa amkabidhi malipo yake.”[13] [Imetolewa na ‘Abd Ar-Razzaaq, na Isnaadi yake ni Munqatwi’ (imekatika). Na Al-Bayhaqiyy ameipokea kwa Isnaadi Mawsuwl (iliyounga) kutoka kwa Abuu Haniyfah.

 

[1] Kumpa mtu kazi ya kumwagilia mti na kuusimamia na kupata malipo katika hilo huitwa Musaaqaah. Kwa jina lingine huitwa Muzaara’ah. Tofauti baina ya Musaaqaah na Muzaara’ah ni kuwa Musaaqaah ni kwa miti ya matunda, wakati Muzaara’ah ni kwa ajili ya nafaka

 

[2] Kumfanya mtu awe ni mshirika wa faida au kodi inaitwa Ijaarah.

 

[3] Hadiyth hii inatoa dalili y akuwepo kwa Musaaqaah na Muzaara’ah.

 

[4] Hanthwalah bin Qays Az-Zurqi Al-Answaar, ni miongoni mwa watu madhubuti Madiynah, na ni katika tabi’iyna wadogo.

 

[5] Ina maana ya kuwa ardhi ya chini inaweza kuchukuliwa na mafuriko na ardhi ya miinuko ikasalimika na wakati wa ukame ardhi ya chini karibu na maji ikasalimika na ardhi ya kwenye miinuko ikaangamia.

 

[6] Thaabit bin Adhw-Dwahaak Al-Answaar, Abuu Zayd, naye ni katika walioshuhudia Bay’at Ar-Ridhwaan, alikuwa Hudaybiyah mwaka wa sita Hijriyyah. Alifariki katika balaa ya ‘Abdullaah bin Az-Zubayr yakaribia mwaka wa 70 Hijriyyah.

 

[7] Katika kiarabu Muzaara’ah ni kumpa mtu shamba alime malipo yake ni baadhi ya kitakachovunwa. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakukataza hili, bali ardhi ilipokuwa ndogo kwa Answaar na Muhajiriyna walipoongezeka kwa njia ya dharura walilima ardhi kadiri walivyoweza na akawafundisha kuwa wasigawane mazao kwa njia ya ushirika wa Muzaara’ah bali wakodishe kwani Ijaarah inawapunguzia uzito kwa wapangaji au wakodishaji.

 

[8] Jina lililotumika Al-Ijaarah lina maana ya kukodisha ardhi kwa muda maalum, jambo ambalo ni la halaal.

 

[9] Kiarabu neno khabiyth lina maana ya tabia mbaya lakini haina maana ya haraam. Wakati mwingine linatumika kama lina maana ya istiara kwa maana ya bakhili.

 

[10] Hadiyth hii imehimiza kulipa mishahara kwa wakati wake kwa mfanyakazi. Siku hizi watu wengi wanakuwa siyo waadilifu katika miamala yao na si waaminifu katika malipo yao.

 

[11] Hadiyth hii inaeleza kwa uwazi kupokea ujira au mshahara kwa kufundisha kitabu cha Allaah na Hadiyth ni halaal. Mwalimu anayefundisha watu kusoma au kuhifadhi Qur-aan anayo haki ya kuchukua malipo.

 

[12] Ina maana ujira na mashahara kwa mfanyakazi lazima ilipwe mapema. Ambaye hatolipa malipo ya mfanyakazi Allaah atamuadhibu siku ya hukumu.

 

[13] Ina maana ya kuwa ujira kwa mfanyakazi ushughulikiwe mapema ili kuondosha migogoro. Vivyo hivyo, katika mas-ala kama Mudhwaarabah, Salaam, Muzaara’ah, Muwaajarah, n.k. kanuni ile ile iliyotekelezwa na shariy’ah lazima ifanye kazi na watu wote watekeleze na kufuata.

Share