Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kuswali Nyumbani Badala Ya Jamaa Msikitini Kwa Sababu Ya Kuona Hayaa

 

Kuswali Nyumbani Badala Ya Jamaa'ah Msikitini Kwa Sababu Ya  Kuona Hayaa

 

Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Mimi naswali nyumba kwa sababu zifuatazo: Nina hayaa mno japokuwa naswali Swalaah nyingi za ziada (Sunnah) na naomba du’aa kila mara na kumtukuza Allaah. Je, Swalaah yangu nyumbani inakubalika?

 

 

JIBU:

 

Ni wajibu kwako kuswali Jamaa'ah Msikitini. Kuona hayaa inayokufanya uache fardhi ni uoga na haijuzu mtu kuacha yaliyo ya fardhi kwa sababu ya kuona hayaa. Mtu kama huyo lazima ajilazimishe kuswali Jamaa'ah, akiona hayaa siku moja basi hatoona hayaa siku ya pili.

 

Lakini ikiwa huwezi kwenda Msikitini kabisa (kwa dharura ya kishariy'ah) na ukaswali nyumbani basi hakuna dhambi juu yako kwa kuwa hiyo ni sababu ya msingi, na Allaah Anasema:

 

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ  

Basi mcheni Allaah muwezavyo [At-Taghaabun: 16]

 

Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((Nikikuamrisheni jambo kufanya, basi fanyeni kadiri muwezavyo))

[Muslim, Ahmad]

 

 

[Fataawaa Islaamiyyah 2/392]

 

 

Share