04-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Asemayo Ni Wahyi Kutoka Kwa Allaah

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

04-Asemayo Ni Wahyi Kutoka Kwa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): 

 

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾

Na wala hatamki kwa hawaa.

 

 

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]

 

 

Imaam As-Sa’dy amesema: “Yaani matamko yake hayatokani na hawaa (matamanio) ya nafsi yake.”

 

Na katika Hadiyth:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ كُنْتُ أَكْتُبُ كُلَّ شَىْءٍ أَسْمَعُهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أُرِيدُ حِفْظَهُ فَنَهَتْنِي قُرَيْشٌ وَقَالُوا:   "أَتَكْتُبُ كُلَّ شَىْءٍ تَسْمَعُهُ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بَشَرٌ يَتَكَلَّمُ فِي الْغَضَبِ وَالرِّضَا؟" فَأَمْسَكْتُ عَنِ الْكِتَابِ فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَأَوْمَأَ بِأُصْبُعِهِ إِلَى فِيهِ فَقَالَ: ((اكْتُبْ فَوَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ مَا يَخْرُجُ مِنْهُ إِلاَّ حَقٌّ)) السلسلة الصحيحة  4 / 45

 

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr ibn Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilikuwa naandika kila nilichokisia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), nikakusudia kuyahifadhi, lakini Maquraysh walinikataza wakasema:  “Je, unaandika kila unachomsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ni bin Aadam tu anaongea kwa ghadhabu na kwa furaha?” Nikaacha kuandika kisha nikamtajia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaashiria kidole chake mdomoni mwake akasema: ((Andika! Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi mwake, hakuna kinachotoka humu isipokuwa haki)) [Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (4/45) (1032)]

 

Na Wahyi ni aina tatu kama walivyosema ‘Ulamaa akiwemo Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) katika Majmuw’ Fataawaa: Kwanza ni Maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Qur-aan. Pili ni Maneno ya Allaah ('Azza wa Jalla) katika Hadiyth Al-Qudsiy na tatu ni maneno ayasemayo yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo Allaah ('Azza wa Jalla) Anamfunulia Wahyi nayo ni katika Hadiyth zilizothibiti usahihi wake, kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾

Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari. [An-Nahl: 44]

 

Kwa maana: Imeteremshwa Al-Quraan ili iwe wazi kufahamika kwa watu yale ambayo yamefichika maana zake na hukmu zake. [At-Tafsiyr Al-Muyassar]

 

Naye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ مَعَهُ)) صحيح رواه أبو داود

((Hakika mimi nimepewa Qur-aan na mfano wake)) [Hadiyth Swahiyh, Abuu Daawuwd]

 

Share