05-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Katumwa Kuwa Ni Rahmah Kwa Ulimwengu

Fadhila Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

05-Katumwa Kuwa Ni Rahmah Kwa Ulimwengu

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٧﴾

Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni rahmah kwa walimwengu. [Al-Anbiyaa: 107]

 

 

Ibn ‘Abaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: “Allaah Amemtuma Nabiy Wake Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni rahmah kwa ulimwengu mzima; Waumini na makafiri. Ama Muumini miongoni mwao ni ambaye Allaah Amemwongoza kupitia kwake na Akamwingiza Jannah (Peponi) kwa sababu ya kumwamini kwake, na kwa kufanyia kazi yale aliyokuja nayo kutoka kwa Allaah. Ama kafiri ni vile kucheleweshewa balaa(na adhabu) ambazo zilikuwa zikawateremkea ummah za awali zilizokanusha waliowafikishia Risala kabla yao.” [Tafsiyr Atw-Twabariy, Ibn Kathiyr]

 

 

Rahmah kwa Waumini pia ni vile kuwatoa kutoka katika kiza na kuwaingiza katika mwanga kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

رَّسُولًا يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِ اللَّـهِ مُبَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ قَدْ أَحْسَنَ اللَّـهُ لَهُ رِزْقًا﴿١١﴾

Ni Rasuli anakusomeeni Aayaat za Allaah zinazobainisha; ili kuwatoa wale walioamini na wakatenda mema kutoka kwenye viza kuingia katika Nuru. Na yeyote anayemwamini Allaah na akatenda mema, Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo abadi. Allaah Amekwishamfanyia rizki nzuri kabisa. [Atw-Twalaaq: 11]

 

Na mifano katika Hadiyth:

 

 عَنْ عَمْرِو بْنِ أَبِي قُرَّةَ، قَالَ كَانَ حُذَيْفَةُ بِالْمَدَائِنِ فَكَانَ يَذْكُرُ أَشْيَاءَ قَالَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لأُنَاسٍ مِنْ أَصْحَابِهِ فِي الْغَضَبِ فَيَنْطَلِقُ نَاسٌ مِمَّنْ سَمِعَ ذَلِكَ مِنْ حُذَيْفَةَ فَيَأْتُونَ سَلْمَانَ فَيَذْكُرُونَ لَهُ قَوْلَ حُذَيْفَةَ فَيَقُولُ سَلْمَانُ: "حُذَيْفَةُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُ" فَيَرْجِعُونَ إِلَى حُذَيْفَةَ فَيَقُولُونَ لَهُ:  "قَدْ ذَكَرْنَا قَوْلَكَ لِسَلْمَانَ فَمَا صَدَّقَكَ وَلاَ كَذَّبَكَ" ‏.‏ فَأَتَى حُذَيْفَةُ سَلْمَانَ وَهُوَ فِي مَبْقَلَةٍ فَقَالَ: "يَا سَلْمَانُ مَا يَمْنَعُكَ أَنْ تُصَدِّقَنِي بِمَا سَمِعْتُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم؟" فَقَالَ سَلْمَانُ: "إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَغْضَبُ فَيَقُولُ فِي الْغَضَبِ لِنَاسٍ مِنْ أَصْحَابِهِ وَيَرْضَى فَيَقُولُ فِي الرِّضَا لِنَاسٍ مِنْ أَصْحَابِهِ ،   أَمَا تَنْتَهِي حَتَّى تُوَرِّ ثَ رِجَالاً حُبَّ رِجَالٍ وَرِجَالاً بُغْضَ رِجَالٍ وَحَتَّى تُوقِعَ اخْتِلاَفًا وَفُرْقَةً وَلَقَدْ عَلِمْتَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم خَطَبَ فَقَالَ: ((أَيُّمَا رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي سَبَبْتُهُ سَبَّةً أَوْ لَعَنْتُهُ لَعْنَةً فِي غَضَبِي - فَإِنَّمَا أَنَا مِنْ وَلَدِ آدَمَ أَغْضَبُ كَمَا يَغْضَبُونَ وَإِنَّمَا بَعَثَنِي رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ - فَاجْعَلْهَا عَلَيْهِمْ صَلاَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ))‏ ‏

   

 

‘Amr bin Abiy Qurrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Hudhayfah alikuwa Madaayin akawa anataja mambo ambayo aliyasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa katika ghadhabu kwa watu katika Maswahaba zake. Watu waliomsikia Hudhayfah walikuwa wakimwendea Salmaan na kumwambia mambo aliyoyasema Hudhayfah.  Salmaan akawa anasema: “Hudhayfah anajua zaidi aliyoyasema.” Kisha wao humjibu Hudhayfah na kumwambia: “Tumemtajia Salmaan yale uliyoyasema, lakini hakukusadiki wala hakukukanusha.” Kisha Hudhayfah akamwendea Salmaan ambaye alikuwa katika shamba lake la mboga akasema: “Ee Salmaan, kitu gani kilichokuzuia usinisadikishe uliyoyasikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?” Salmaan akasema: “Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akighadhibika na huwaambia watu kati ya Maswahaba zake (maneno) ya ghadhabu, na huwa katika furaha na hapo huwasemesha watu kwa furaha.  Je, hivi hutoacha mpaka utie mapenzi ya watu katika nyoyo za watu na utie chuki za watu katika nyoyo za watu hadi usababishe watu kukhitilafiana na kufarikiana? Unajua kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikhutubia akasema: ((Ikiwa kuna mtu yeyote katika Ummah wangu ambaye nilimtolea lugha isiyo nzuri nilipokuwa katika ghadhabu au kumlaani - basi hakika mimi ni katika wana Aadam, hughadhibika kama mnavyoghadhibika. Hakika Allaah Amenitumia kuwa ni rahmah kwa walimwengu. (Ee Allaah) Ijaalie (ghadhabu au laana yangu) iwe du’aa (ya kuwatakasa, ujira na kikurubishho kwa Allaah),  Siku ya Qiyaamah)) [Sunan Abiy Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd, As-Silsilah Asw-Swahiyhah, Swahiyh Al-Jaami’

 

 

Ama rahmah kwa makafiri ni kama mfano wa Hadiyth:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ ادْعُ عَلَى الْمُشْرِكِينَ قَالَ: ((إِنِّي لَمْ أُبْعَثْ لَعَّانًا وَإِنَّمَا بُعِثْتُ رَحْمَةً)) مسلم  

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba ilisemwa: Ee Rasuli wa Allaah! Omba du’aa dhidi ya makafiri.” Akasema: ((Hakika mimi sikutumwa kuwa ni mwenye kuomba laana  bali hakika nimetumwa kuwa ni rahmah)) [Muslim]

 

Mfano wa rahmah kwa wanyama ni Hadiyth:

 

عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ:  كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي سَفَرٍ فَانْطَلَقَ لِحَاجَتِهِ فَرَأَيْنَا حُمَّرَةً مَعَهَا فَرْخَانِ فَأَخَذْنَا فَرْخَيْهَا فَجَاءَتِ الْحُمَّرَةُ فَجَعَلَتْ تَفْرُشُ فَجَاءَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: ((مَنْ فَجَعَ هَذِهِ بِوَلَدِهَا رُدُّوا وَلَدَهَا إِلَيْهَا)) ‏.‏ وَرَأَى قَرْيَةَ نَمْلٍ قَدْ حَرَّقْنَاهَا فَقَالَ: ((مَنْ حَرَّقَ هَذِهِ)) ‏.‏ قُلْنَا نَحْنُ ‏.‏ قَالَ: ((إِنَّهُ لاَ يَنْبَغِي أَنْ يُعَذِّبَ بِالنَّارِ إِلاَّ رَبُّ النَّارِ))

 

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Abdillaah kutoka kwa baba yake amesema: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) safarini, akaondoka kwenda kujisaidia. Tukamuona ndege akiwa na (vitoto vyake) viwili vidogo. Tukavichukua vidogo. Yule ndege akaja akawa anatandaza mbawa zake. Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja na akasema: ((Nani aliyemtia majonzi  huyu kwa kwa kumpotezea vidogo vyake? Mrudishieni vidogo vyake)) Akaona pia mdudu chungu wa shamba tuliyemuunguza, akasema: ((Nani kamuunguza?)) Tukasema: “Sisi.” Akasema: ((Hakika haijuzu yeyote kuadhibu kwa moto isipokuwa Rabb wa moto)) [Sunan Abiy Daawuwd (2765), ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd, As-Silsilah Asw-Swahiyhah]  

 

 

Na pia rahmah yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kuchinja wanyama:

 

عَنْ شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ، قَالَ ثِنْتَانِ حَفِظْتُهُمَا عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ كَتَبَ الإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذَّبْحَ وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ فَلْيُرِحْ ذَبِيحَتَهُ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Shaddaad bin Aws (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Mambo mawili nimeyahifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hakika Allaah Ameamrisha kufanya wema katika kila jambo, basi mkiua ueni vizuri, na mkichinja chinjeni vyema, na atie makali kisu chake anayetaka kuchinja ili amuondoshee adhabu kichinjwa chake)) [Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaa’iy, Ibn Maajah na Ad-Daarimiy]

 

Share