09-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Mtu Bora Kabisa, Mkarimu Mno Na Shujaa

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

09-Mtu Bora Kabisa, Mkarimu Mno Na Shujaa

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَنَسٍ، رضى الله عنه قَالَ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم أَحْسَنَ النَّاسِ وَأَشْجَعَ النَّاسِ وَأَجْوَدَ النَّاسِ، وَلَقَدْ فَزِعَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ، فَكَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم سَبَقَهُمْ عَلَى فَرَسٍ، وَقَالَ: ((وَجَدْنَاهُ بَحْرًا))

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa mtu bora kabisa, shujaa kabisa na mkarimo mno kuliko watu wengineo. Pindi watu wa Madiyna walipofazaika (kwa khofu), Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipanda farasi akatangulia mbele yao na akasema: ((Tumempata farasi huyu haraka kabisa))  [Al-Bukhaariy]

 

Na katika Hadiyth nyengine:

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  أَحْسَنَ النَّاسِ وَكَانَ أَجْوَدَ النَّاسِ وَكَانَ أَشْجَعَ النَّاسِ وَلَقَدْ فَزِعَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ ذَاتَ لَيْلَةٍ فَانْطَلَقَ نَاسٌ قِبَلَ الصَّوْتِ فَتَلَقَّاهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَاجِعًا وَقَدْ سَبَقَهُمْ إِلَى الصَّوْتِ وَهُوَ عَلَى فَرَسٍ لِأَبِي طَلْحَةَ عُرْيٍ فِي عُنُقِهِ السَّيْفُ وَهُوَ يَقُولُ" ((لَمْ تُرَاعُوا لَمْ تُرَاعُوا)) قَالَ: ((وَجَدْنَاهُ بَحْرًا)) أَوْ ((إِنَّهُ لَبَحْرٌ)) .‏ قَالَ: وَكَانَ فَرَسًا يُبَطَّأُ   مسلم  
 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa mtu bora kabisa, na mkarimu mno kuliko watu wengineo, na shujaa kabisa. Usiku mmoja, watu wa Madiynah walifazaika kwa khofu (ya mshindo wa sauti). Wakatoka watu kuelekea mshindo wa sauti lakini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alishafika kabla yao sehemu ya sauti hiyo, akakutana nao akasema: ((Msikhofu! Msikhofu!)) Naye alikuwa amepanda farasi wa Abuu Twalhah, farasi huyo alikuwa hana tandiko lake  na shingoni mwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  kulikuwa na panga akasema: ((Nimeshampata farasi kwa haraka kama (kasi ya mawimbi ya) bahari)) Au ((Hakika hiyo (sauti ya mshindo) ni (mfoko wa) bahari)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share